Habarika | ZAIDI YA KAYA 350 WILAYANI KILOSA ZIMEATHIRIKA KWA MAFURIKO
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

ZAIDI YA KAYA 350 WILAYANI KILOSA ZIMEATHIRIKA KWA MAFURIKO

Zaidi ya kaya 373 katika kijiji cha Mambegwa wilayani Kilosa  hazina makazi baada ya nyumba walozokuwa wakiishi kuzingirwa na maji huku nyumba zaidi ya 50 zikibomoka kabisa kutoka na mafuriko yanayosababishwa na mvua kubwa na za upepo zinazoendelea katika mkoa wa morogoro.

Kituo cha televisheni cha ITV kimefika kijijini hapo na kushuhudia nyumba zikiwa zimebomoka na nyingine kuzingirwa na maji,huku baadhi ya wananchi walioathirika wakifanya jitihada za kuokoa baadhi ya mali zilizonusurika na kuhamia katika shule ya msingi Mambegwa iliyopo maeneo ya mlimani ambapo wamesema kwa sasa hali ni mbaya baada ya vyakula na mali zao nyingi kusombwa na maji hivyo kuiomba serikali kuwapatia maeneo ya juu ambayo kwa sasa ni mashamba pori yaliyotelekezwa na wawekezaji ili wapate maeneo salama ya kuishi.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mambegwa Said Ally  amesema tayari serikali ya kijiji imejulisha mamlaka za juu  athari hizo,na kwamba vyakula vyote walivyopewa msaada hivi karibuni na serikali navyo vimesombwa na maji hivyo na kuwataka wananchi wote ambao bado wako katika maeneo hayo kufanya maaamuzi ya kuondoka mapema ili kuepusha athari kubwa zaidi kujitokeza.
-ITV
Sambaza Makala hii: Share on Facebook5Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By