Habarika | WIZARA YA FEDHA KUSIMAMIA MAUZO YA KOROSHO NA UFUTA
layout-wrap boxed
Friday, April 27, 2018

WIZARA YA FEDHA KUSIMAMIA MAUZO YA KOROSHO NA UFUTA

Wizara ya Fedha na Mipango kupitia mamlaka ya Masoko, Mitaji na Dhamana (CMSA) mkoani Lindi itasimamia mauzo ya korosho na ufuta katika mfumo wa stakabadhi kwa msimu wa mwaka huu.

Meneja wa uhusiano wa CMSA, Charles Shirima, alisema hali hiyo itaweza kuondoa migongano baina ya wakulima, vyama vya msingi vya ushirika na wanunuzi, wakati wa mauzo ya mazao hayo na malipo.

Shirima alisema hayo wakati alipokuwa akiitambulisha taasisi hiyo ya serikali kwa viongozi wa ngazi ya ofisi ya mkuu wa mkoa, wilaya, makundi ya wakulima, kamati ya muda ya chama Kikuu cha Ushirika Lindi mwambao juu ya kusimamia kimauzo mazao hayo katika msimu wa mwaka huu.

Shirima alisema uanzishwaji wa soko la bidhaa utaweza kuleta mawasiliano na sekta za fedha, miundombinu na mfumo wa stakabadhi kwa baadhi ya mazao.

Alisema kwamba maendeleo hayo yanatoa fursa za kuboresha mfumo wa masoko nchini ili kuleta mfumo wenye ushindani na ulio wazi na ambao utaweza kumfanya mkulima aweze kunufaika na juhudi zake.

Kwa mujibu wa Shirima, kuondoa migongano kutaweza kuleta chachu kwa wakulima kuweza kuzalisha kwa wingi kutokana na kuwepo kwa masoko mbalimbali ya mazao hayo.

Naye mchambuzi wa fedha wa mamlaka hiyo, Witness Gowelle alisema mamlaka hiyo isimamie kwa mara ya kwanza kwa mazao ghafi na kutafutiwa masoko.

-HABARI LEO

Sambaza Makala hii: Share on Facebook2Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By