Habarika | WATOTO WACHANGA WATUMIKA KUTEKELEZA MATUKIO YA KUJILIPUA MHANGA YA BOKO HARAM
layout-wrap boxed
Tuesday, May 22, 2018

WATOTO WACHANGA WATUMIKA KUTEKELEZA MATUKIO YA KUJILIPUA MHANGA YA BOKO HARAM

Wanawake wanaojitoa mhanga nchini Nigeria wameanza kutumia watoto kuepuka vizuizi vya ukaguzi, jambo ambalo, serikali nchini humo inasema linaweza kuwa mwelekeo wa hatari.

Tahadhari hiyo imekuja baada ya wanawake wawili waliokuwa wamebeba watoto mgongoni kufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga katika mji wa Madagali siku 10 zilizopita.

Januari 13 mwaka huu, wanawake wanne waliokuwa wakijitoa mhanga walifika kwenye mji wa Maddaggalee katika jimbo la Adamawa, wawili walitambuliwa na walinzi waliokuwa katika vizuizi na kutakiwa kusimama, baada ya mbinu zao kugundulika.

Lakini wengine wawili walifanikiwa kupita bila ya kugunduliwa. kubeba kwao watoto kulifanya wasigunduliwe na kuweza kusababisha maafa yaliyosababisha vifo vya watu wanne, wao wenyewe kufariki na watoto wawili pia waliokuwa wamewabeba katika mawili tofauti.

Kundi la Boko Haram linajulikana kwa kuwatumia wanawake, hususan wasichana katika mabomu ya kujitoa mhanga, Hata hivyo ni mara ya kwanza katika maasi hayo kutumia watoto wachanga.

 

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By