Habarika | WANAUME NCHINI CHINA WACHUKIZWA NA HUDUMA YA BASI LA WANAWAKE PEKEE.
layout-wrap boxed
Tuesday, May 22, 2018

WANAUME NCHINI CHINA WACHUKIZWA NA HUDUMA YA BASI LA WANAWAKE PEKEE.

Uzinduzi wa basi la wanawake pekee katika mji mmoja wa China umewakasirisha wanaume wa taifa hilo na kuzua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii.

Huduma hiyo mpya itatolewa wakati wa asubuhi na wakati wa shughuli nyingi katika mji wa mashariki wa Zhengzhou katika juhudi za kupunguza matukio ya wanawake kusumbuliwa na wanaume kulingana na gazeti la Dahe daily.

Kampuni hiyo ya mabasi itawalinda wanawake dhidi ya kunyanyaswa wakati wanapovaa nguo nyepesi huku wanawake wanaonyonyesha wakihisi wapo salama.

Treni za wanawake na mabasi yameanzishwa katika mataifa mengi na kuonyesha ufanisi mkubwa, lakini magari ya uchukuzi ya watu wa jinsia moja ni swala jipya nchini Uchina.

Wanawake waliohojiwa ndani ya basi hilo wanasema wanafurahishwa na huduma hiyo huku mmoja akimwambia ripota kwamba ni heshima kubwa kwa wanawake licha ya baadhi ya wanaume hawafurahii jambo hilo.

Mwanamume mmoja aliliambia gazeti la Dahe Daily kwamba unyanyasaji sio jambo la kawaida katika magari ya uchukuzi kwamba kampuni ya basi hilo imewakejeli na kuwafedhehesha wanaume.

Mtu mwengine amelalamika katika kituo cha redio cha Uchina kwamba alilazimika kungojea sana kwa basi jingine kuwasili kwa kuwa hakuruhusiwa ndani.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook1Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By