Habarika | WANAJESHI WA URUSI WAANZA KUONDOKA SYRIA
layout-wrap boxed
Tuesday, May 22, 2018

WANAJESHI WA URUSI WAANZA KUONDOKA SYRIA

Wanajeshi wa Urusi wameanza kuondoka Syria siku moja baada ya Rais Vladimir Putin kushangaza wengi kwa kutangaza kwamba wanajeshi wa nchi yake wangeondoka nchini humo.

Kundi la kwanza la ndege za kivita za nchi hiyo limeondoka kutoka kambi ya Hmeimim nchini Syria mapema asubuhi, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema.

Mataifa ya Magharibi yamefurahia hatua hiyo, ingawa kwa tahadhari, yakisema itaishinikiza serikali ya Syria kushiriki kwenye mazungumzo ya amani yanayolenga kumaliza mzozo nchini humo ambayo yameingia siku yake ya pili leo.

Hayo yakijiri, tume ya Umoja wa Mataifa inatarajiwa kutoa ripoti ya kutekelezwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita nchini Syria baadaye leo.

Hatua ya kuondolewa kwa baadhi ya wanajeshi wa Urusi nchini Syria ilitangazwa Jumatatu wakati wa mkutano kati ya Bw Putin na mawaziri wake wa ulinzi na mashauri ya kigeni ambapo Putin alisema majeshi hayo yametimiza lengo lililokusudiwa.

Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin

 

Urusi ni mshirika mkubwa wa Rais wa Syria Bashar al-Assad, na ofisi yake imejaribu kuondoa uvumi kwamba kumezuka tofauti baina ya nchi hizo mbili, na kusema uamuzi huo ulifikiwa kwa pamoja.

Operesheni ya kijeshi ya Urusi ilianza Septemba mwaka jana na kuisaidia sana serikali ya Syria ambayo ilifanikiwa kukomboa maeneo kutoka kwa waasi.

Kwa mujibu wa waziri wa ulinzi Sergei Shoigu, kama alivyonukuliwa na vyombo vya habari vya Urusi, ndege za kivita za taifa hilo lilifanya safari 9,000 na kusaidia kukombolewa kwa maeneo 400 ya makazi.

Jeshi la Urusi, amesema Bw Shoigu, lilisaidia serikali ya Bw Assad kukomboa eneo la kilomita mraba 10,000.

-BBC SWAHILI

Sambaza Makala hii: Share on Facebook2Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By