Habarika | WALENGWA WA TASAF BUKOBA WAOMBA KUONGEZEWA RUZUKU
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

WALENGWA WA TASAF BUKOBA WAOMBA KUONGEZEWA RUZUKU

Walengwa walioko mpango wa kunusuru kaya masikini waliko mitaa ya Rubumba na KagondoKaifo kata za Nyanga na Kagondo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera,wameiomba serikali kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii(TASAF)kuongeza kiwango cha ruzuku kwa mlengwa,lengo kufanikisha madhumuni yaliyokusudiwa ya kuhakikisha kaya masikini sana zinaondokana na umasikini.

Rai hiyo,imetolewa na walengwa hayo kwa nyakati tofauti wakati wa matembezi ya Katibu tawala wa Mkoa wa Kagera Amantius Msole,alipokuwa akiwatembelea walengwa wa mpango huo ili kujionea maendeleo ya miradi yao walioanzisha kutokana na ruzuku wanayopokea kwa kila mwezi kwa lengo la kuondokana na umasikini.
Devotha Fella(35)mkazi wa mtaa wa Rubumba,pamoja na shukrani kwa serikali juu ya utekelezaji wa mpango huo,aliomba Serikali kupitia mfuko huo,kufikiria ni jinsi gani inaweza kuongeza kiwango cha ruzuku kutoka 20,000/=inayotolewa kwa ajili ya kujikimu,kutokana gharama za uendeshaji wa maisha kupanda.
Amesema iwapo kiwango hicho kitaongezeka,kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo mabadiliko makubwa baina ya walengwa kutoka kwenye hali ya umasikini kufikia hali ya kawaida ya maisha ya kati kwani mbali na kiwango kinachotolewa kwa sasa kuwa kidogo lakini kimewezesha kusaidia kuwepo kwa mabadiriko ya maisha kwa walengwa hao.
Katika ziara hiyo iliyolenga kuwatembelea walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini Manispaa ya Bukoba, Katibu Tawala mkoa wa Kagera Amantius Msole alitembelea walengwa katika mitaa ya Rubumba na Kagondo Kaifo yote hipo Manispaa ya Bukoba na kushuhudia miradi ya ufugaji na ujasiliamali iliyoanzishwa na baadhi ya walengwa hao.
-ITV
Sambaza Makala hii: Share on Facebook2Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By