Habarika | MAMIA YA WAHINDI WAONGOZA MAANDAMANO YA KUPINGA UBAGUZI.
layout-wrap boxed
Sunday, February 25, 2018

MAMIA YA WAHINDI WAONGOZA MAANDAMANO YA KUPINGA UBAGUZI.

Kufuatia tukio la kibaguzi lililotokea nchini India kwa mwanafunzi wa Kitanzania kufanyiwa tukio la udhalilishaji mbele ya umati wa watu, mamia ya wakazi wa huko Bridage Road ambapo tukio hilo limetokea, wamejitokeza kuongoza maandamano ya kupinda ubaguzi katika eneo hilo.

Maandamano hayo yamekuja baada ya mwanafunzi wa kike kutoka nchini Tanzania anayesoma nchini humo kudhalilishwa kwa kuvuliwa nguo zake na kuchomewa gari lake moto na raia wa eneo hilo wenye hasira kali baada ya mwanamke mmoja kugongwa na kufa papo hapo na mwanafunzi mwingine anayetokea nchini Sudan.

Kitendo hicho kimetafsiriwa kuwa ni ubaguzi wa rangi hasa baada ya raia hao wa India kuonekana kama wanataka kulipa kisasi kwa wanafunzi wote wa kiafrika wanaosoma maeneo yao hasa baada ya mmoja wa wanafunzi hao wa kiafrika kutoka nchini Sudan kumgonga na kumuua mwanamke wa kihindi aliyekuwa amelala pembezoni mwa barabara hivyo.

Hata hivyo kumekuwa mawazo gongana juu ya taarifa hiyo baada ya mwanafunzi huyo wa kitanzania kudai kuwa baada ya kufanyiwa unyama huo alifanikiwa kutoroka na kwenda kituo cha polisi cha karibu kwa ajili ya kufungua jalada la kesi huku polisi wakikataa kumfungulia jalada hilo. Lakini hata hivyo Kamishna wa polisi wa Bangalore alikanusha taarifa hizo na kudai kuwa polisi ndio walikuja kumuokoa mwanafunzi huyo mikononi mwa raia hao wenye hasira kali.

Kumekuwa na mjadala mzito katika mitandao ya kijamii baina ya wanafunzi wa Kiafrika wanaosoma nchini India huku wakilaani vikali tukio hilo la kusikitisha na kudai kuwa hawana amani tena kuishi nchini humo. Lakini katika hali ya kuonyesha kusikitishwa na tukio hilo la kibaguzi, mamia ya raia wa Bangalore nchini India wameongoza maandamano wakiungana na wanafunzi hao wa kiafrika katika kukemea ubaguzi huo.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like


Warning: file_get_contents(http://graph.facebook.com/?ids=http://habarika.com/wahindi-waongoza-maandamano-ya-kupinga-ubaguzi/): failed to open stream: HTTP request failed! HTTP/1.1 403 Forbidden in /home/habarika/public_html/wp-content/themes/habarika/elements/element.php on line 80
0 comments

By