Habarika | WAANDISHI WASHAURIWA KUUNDA BODI YA WATAALAMU KUSIMAMIA MAADILI
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

WAANDISHI WASHAURIWA KUUNDA BODI YA WATAALAMU KUSIMAMIA MAADILI

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuunda bodi ya wataalamu waliobobea ambayo itasimamia maadili ya taaluma hiyo na kuchukua hatua kwa mwanataalumayeyote anayekiuka maadili.

Hayo yalisema jijini Dar es Salaam na Mdhadhiri wa Chuo Kikuu Huria, Dk Hamza Kondo wakati akizindua kitabu chake kinachohusu masuala ya uandishi wa habari kinachoitwa “Uandishi Huru Tanzania ni Mapambano ENdelevu”

Alisema fani yoyote ya taaluma duniani ili iheshimike ni lazima iwe na bdoi hivyo kuwepo kwa bodi ya waandishi wa habari kutasaidia taaluma hiyo kuheshimika nchini na duniani kote.

Alisema kitabu hicho ni zao la utafiiti wa miaka mitano uliofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa na Mtwara.

Alisema uandishi wa kitabu hicho ulishirikisha wananchi wa vijiji kutoka kata nane za wilaya hizo na wadau wa habari 994 wakiwemo kutoka mihimili mitatu ya dola  ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama

Pia alisema asasi mbili za Kiraia zilizshiriki huku moja ikiwa ya wanahabari na nyingine ya wanaharakati za haki za binadamu.

Kwa upande wa wanahabari walioshiriki ni Klabu ya Waandishi ya Iringa na kwa wanaharakati, ulishiriki Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)

Wakati huohu amewaasa waandishi wa habari kujiendeleza kielimu katika fani ya uandishi wa habari na taaluma nyingine ili waweze kukabiliana na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.

Mbali na hayo, Dk Kondo ametoa zawadi ya vitabu kwa baadhi ya vyombo vya habari nchini likiwemo gazeti la Jamhuri, Majira, HabariLeo, Mwananchi na Nipashe.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook1Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By