Habarika | UTABIRI WA T.B JOSHUA WAMTIA KIBULI LOWASSA: ATAMBA KUINGIA IKULU 2020 BILA KUMWAGA DAMU
layout-wrap boxed
Sunday, February 25, 2018

UTABIRI WA T.B JOSHUA WAMTIA KIBULI LOWASSA: ATAMBA KUINGIA IKULU 2020 BILA KUMWAGA DAMU

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema ataingia Ikulu baada ya miaka minne ijayo na rafiki yake T.B Joshua amemtabiria kuwa serikali ijayo itaongozwa na Chadema

Akizungumza na viongozi na wanachama wa Chadema mkoani Tabora, mjumbe huyo alisema ana uhakika wa kuingia Ikulu bila ya umwagaji wa damu.

Baada ya kutoa kauli hiyo alishangiliwa na kuwashukuru wana Tabora na Watanzania kwa ujumla kwa kura walizompa katika uchaguzi mkuu uliopita. Alieleza kuwa mhubiri huyo maarufu barani Afrika anayefanya shughuli zake nchini Nigeria na ambaye alikuja nchini mara baada ya Uchaguzi Mkuu uliopita, alimpa angalizo kuwa ili washinde ni lazima wawe wamoja, washikamane na kuwa majasiri.

“Najua waandishi wa habari wataandika, lakini sijali rafiki yangu Joshua ametabiri serikali ijayo ya Tanzania itaongozwa na Chadema,” alisema Lowassa.

Ikumbukwe Lowassa alishika nafasi ya pili katika kinyang’anyiro cha urais mwaka jana na ameshaonyesha nia ya kuingia tena kwenye mpambano huo wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook3Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By