Habarika | URUSI YAZUIWA KUPELEKA WANARIADHA KWENYE MICHUANO YA OLIMPIKI YA RIO
layout-wrap boxed
Friday, April 27, 2018

URUSI YAZUIWA KUPELEKA WANARIADHA KWENYE MICHUANO YA OLIMPIKI YA RIO

Wanariadha wa Urusi hawatashiriki michezo ya Olimpiki ya mwaka huu huko Brazil.

Kauli hiyo imeafikiwa na mahakama ya juu ya michezo ambayo imefutilia mbali rufaa iliyowasilishwa na kamati ya olimpiki ya Urusi ROC ya kuitaka ibatilishe uamuzi wa shirikisho la riadha duniani IAAF ya kuwapiga marufuku wanariadha wake wote wasishiriki michezo ya olimpiki itakayoandaliwa jijini Rio De Jenairo Brazil kuanzia mwezi ujao.

IAAF ilifikia uamuzi huo baada ya kugundulika kuwa serikali ya Urusi ilikuwa na mpango wa chini kwa chini wa kuficha matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku miongoni mwa wanariadha wake.

Kamati ya olimpiki ya Urusi ilikuwa imekata rufaa kwa pamoja na takriban wanariadha 68 ambao hawajawahi kupatikana na hatia ya matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu mwilini.

Baada ya kusikiza pande zote mbili mahakama hiyo ya juu katika riadha CAS imeamua kufutilia mbali rufaa hiyo ambapo kauli hiyo imewadia siku moja tu baada ya uchunguzi huru kubaini kuwa wizara ya michezo ya Urusi, na kamati ya kupambana na matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini ya Urusi zilishiriki udanganyifu ikiwemo kubadilisha mikojo yawanariadha ili vipimo visipatikane na madawa hayo yaliyopigwa marufuku.

Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa IOC imesema itatathmini kwanza hatua za kisheria, kabla ya kufanya uamuzi wowote kuhusu iwapo itaipiga marufuku Urusi kutoshiriki kwenye mashindano ya Olimpiki huko Rio de Janeiro Brazil.

Hatua hii inafuatia ripoti huru kuhusu serikali kuhusika na kuwasaidia wanamichezo wake katika matumizi ya madawa ya kusisimua misuli.

IOC hata hivyo imewafungia maafisa wote wa Urusi kushiriki michuano ya Olimpiki ya Rio, na itawapima tena wanamichezo walioshiriki michuano ya Olimpiki ya majira ya baridi yaliyofanyika Sochi huku tayari wanariadha wa Urusi wakiwa  wamepigwa marufuku na IAAF.

Shirikisho la riadha IAAF limefurahia kauli hiyo ya mahakama ya juu ya michezo ikisema kuwa imesawazisha uwanja wa riadha.

”Kwa hakika tumefurahi kuwa CAS imeunga mkono kauli yetu. Leo kwa hakika sio siku ya kufurahia kwani IAAF haikuja katika michezo kuwazuia wanariadha wasishiriki katika michezo ila nia yetu ni kusawazisha uwanja ili wanariadha wote washindane kwa mizani sawa” alisema rais wa shirikisho la riadha Lord Sebastian Coe.

”Baada ya Rio tutaendelea kuisaidia kamati ya olimpiki ya Urusi ili kuwaruhusu wanariadha wake kurejea katika mashindano ya kimataifa.” aliongezea Coe.

Licha ya uamuzi huo wa CAS, wanariadha wachache wa urusi ambao watakubali kushiriki chini ya bendera ya kamati ya olimpiki wataruhusiwa kushiriki ila lazima wapitie vipimo za ziada ilikuthibitisha kuwa ni wasafi.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook1Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By