Habarika | WHO: UGONJWA WA ZIKA HAUTALETA MADHARA KWENYE MICHUANO YA OLIMPIKI BRAZIL
layout-wrap boxed
Friday, April 27, 2018

WHO: UGONJWA WA ZIKA HAUTALETA MADHARA KWENYE MICHUANO YA OLIMPIKI BRAZIL

Shirika la afya duniani linasema mikusanyiko mikubwa wakati wa kipindi cha michuano ya Olimpiki nchini Brazil haina maana kwamba washiriki wako hatarini kuambukizwa virusi vya zika.

Kamati ya dharura ya WHO juu ya ugonjwa wa ZIKA ilikutana Jumanne ya jana ili kuangalia uwezekano wa hatari katika mikusanyiko mikubwa ya watu katika miji na nchi iliyo na mlipuko wa ZIKA ikiwa ni pamoja na Rio De Janeiro.

Kamati hiyo ilieleza hatari ya mtu mmoja mmoja katika maeneo ya maambukizo iko sawa bila kujali kuna mkusanyiko au la na inaweza kupungua kwa kufuata masharti ya afya.

Idara hiyo ya umoja wa mataifa inasema kuna hatari ndogo kwamba michuano ya olimpiki ya mwezi Agost inaweza kusambaza Zika kimataifa.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook3Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By