Habarika | TRUMP AZICHIMBA MKWARA MZITO KAMPUNI ZINAZOTAKA KUONDOKA MAREKANI
layout-wrap boxed
Tuesday, December 12, 2017

TRUMP AZICHIMBA MKWARA MZITO KAMPUNI ZINAZOTAKA KUONDOKA MAREKANI

donald

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amezionya kampuni dhidi ya hatua kali iwapo zitaondoka Marekani.

Alikuwa akizungumza katika jimbo la Indiana ambapo alijisifu kwa kunusuru kazi 1000 katika kampuni ya Carrier Corp ambayo ilikuwa inapanga kuhamia Mexico.

Bw Trump sasa yuko katika jimbo la Ohio kuanza ziara ya kutoa shukrani kwa wafuasi wake.

Kiongozi huyo aliunga mkono mazungumzo na kampuni ya Carrier Corp kama mfano wa vile atakavyoshirikiana na wafanyibiashara wengine wanaotaka kuhamia mataifa mengine.

”Tutakuwa na hali ambapo wataelezwa kwamba tutawachukulia vyema na pia kutakuwa na hatua kali dhidi yao”,alisema.

”Watalipishwa kodi za viwango vya juu katika mpaka iwapo wanataka kuondoka”.

Pia aliahidi mpango wake wa kampeni wa kupunguza kodi miongoni mwa biashara nchini Marekani.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook3Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn1Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By