Habarika | TRUMP AMTUHUMU CLINTON KWA UBAGUZI NA MAUAJI YANAYOENDELEA NCHINI MAREKANI
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

TRUMP AMTUHUMU CLINTON KWA UBAGUZI NA MAUAJI YANAYOENDELEA NCHINI MAREKANI

Mgombea urais wa Marekani kupitia Chama cha Republican Donald Trump ambaye yupo katika mji wa Milwaukee amesema ushahidi wa awali unaonyesha kuwa ilikuwa ni halali kijana mweusi aliyeuawa na polisi katika mji huo siku ya jumamosi.

Mauaji ya kijana huyo Syville Smith ambayo yalitokea katika mji huo Milwaukee wenye wamarekani wengi wenye asili ya Afrika na kusababisha maandamano makubwa hivi karibuni.

Katika kampeni hiyo Trump amemshambulia mpinzani wake Hilary Clinton kwamba amechangia kuwepo kwa vurugu katika mji huo.

“Utekelezaji wa sheria, kujumuisha jamii , utendaji bora wa polisi ni mambo ambayo nchi yetu inahitaji.

Kama vile mgombea urais wa Hilary Clinton yeye alikuwa hawajali watu wa hali wa chini alikuwa anawapinga polisi mniamini mimi. Hayo yamekuwa yakihamasisha uhalifu kama ubaguzi kwenye jamii yetu mambo ambayo yamekuwa yakichochewa na mpinzani wangu ambaye ameshiriki moja kwa moja vurugu za Milwaukee na maeneo mengine katika nchi yetu.” Alisema.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook2Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By