Habarika | TRUMP AHOFIWA KUISAMBARATISHA REPUBLICAN
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

TRUMP AHOFIWA KUISAMBARATISHA REPUBLICAN

Wakuu wa chama cha Republican wanasema ikiwa watamruhusu Donald Trump awe mgombea urais kuna uwezekano mkubwa wa chama hicho kusambaratika.

Mmoja ya vigogo hao wa Republican, Seneta Lindsey Graham wa South Carolina anasema njia ya pekee ya kumzima tajiri huyo , Donald Trump ni wanachama kumuunga mkono mgombea mwengine wa Republican Bw Ted Cruz.

Aliyekuwa mgombea urais wa chama katika uchaguzi wa miaka mmine iliyopita Bw Mitt Romney pia anasema Bw Trump hafai kuwa mgombea wao japo hadi sasa ameshinda katika majimbo mengi katika kura ya mchujo.

Sasa kibarua kigumu mbele ya wakuu wa Republican ni vipi watamuondoa Bw Trump bila ya kuwakasirisha wafuasi wake ambao wengine ni wa chama cha Demokratic. Endapo kamaTrump atanyimwa tiketi ya chama cha Republican basi anaweza kuamua kugombea urais kama mgombea huru asiyekuwa na chama.

Hii inatokana na utafiti wa hivi punde unaonyesha kuwa ikiwa Hillary Clinton wa Democratic atasimama na Donald Trump basi utakuwa ni mpambano mkali, hivyo kumjua nani kati yao atashinda urais itakuwa vigumu.

David Merritt wa shirika moja la kutafiti na kutoa ushauri kwa wagombea urais anasema mtu anayemuweza Hilary Clinton ni Bw Trump na anayemuweza tajiri huyo ni Bi Hillary Clinton.

Lakini kadiri siku zinavyo songa mbele hatima ya Donald Trump ndani ya Chama cha Republican itajulikana, kwani tayari mgombea mmoja wa chama cha Republican Ben Carson amesema atajiondoa katika mchuano huo akisema anaweka maslahi ya Wamarekani mbele kuliko yake binafsi.

-BBC SWAHILI

Sambaza Makala hii: Share on Facebook2Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By