Habarika | TANZANIA NI MIONGONI MWA NCHI ZINAZOONGOZA AFRIKA KWA WAGONJWA WA MOYO
layout-wrap boxed
Saturday, March 24, 2018

TANZANIA NI MIONGONI MWA NCHI ZINAZOONGOZA AFRIKA KWA WAGONJWA WA MOYO

Tanzania ni miongoni mwa nchi barani Afrika zinazoongoza kwa wagonjwa wenye matatizo ya Moyo kufuatia idadi kubwa ya wananchi kubadili mifumo ya maisha ikiwemo kutokufanya mazoezi na kupelekea kuwa na shinikizo la damu.

Hayo yamebainisha jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano uliowakutanisha madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka nchi mbalimbali barani Afrika ambapo mganga mkuu wa serikali nchini Tanzania amesema jitihada za serikali hazitazaa matunda kama watanzania hawatakuwa tayari kuzuia tatizo badala ya kutibu tatizo.
Rais wa chama cha madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo nchini Docta Robert Mvungi amsema mkutano huo unalenga kuchambua matatizo yanayopelekea magonjwa hayo yanayogharimu maisha ya watu ili kuona namna ya kutoa elimu na hatimae kupunguza magonjwa hayo.
Kaimu Mkurugenzi wa taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete amesema licha ya taasisi hiyo kuendelea kupunguza kwa asilimia kubwa wagonjwa kwenda kutibiwa nje bado tatizo hilo kwa Tanzania limeendelea kuwa kubwa na kubaini ni vyema watanzania wakaweka mazoea ya kupima afya zao mara kwa mara ili kugundulika mapema na kuweza kutibiwa.
CHANZO: ITV
Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By