Habarika | SUMATRA: HIVI NDIVYO DARAJA LA KIGAMBONI LITAKAVYOUNGANISHA JIJI LA DAR
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

SUMATRA: HIVI NDIVYO DARAJA LA KIGAMBONI LITAKAVYOUNGANISHA JIJI LA DAR

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imeanzisha njia mpya ya usafiri wa daladala kati ya Kigamboni na maeneo mengine jijini Dar es Salaam. Ilianza juzi kutoa leseni kwa mabasi ya daladala yanayobeba abiria kati ya Kigamboni – Machinga Complex iliyoko Ilala, Temeke na Mbagala Rangi Tatu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Mawasiliano ya Umma ya Sumatra, njia hizo zimeanzishwa kutokana na kufunguliwa kwa Daraja la Mwalimu Nyerere linalounganisha Kigamboni na maeneo mengine ya jiji hilo kwa barabara.

Sumatra imewataka wamiliki wa mabasi yanayofanya safari hizo na wawekezaji katika sekta hiyo kuwasilisha maombi ya leseni katika ofisi zao mkoa wa Dar es Salaam. Imewataka kuwa na madereva na makondakta watakaozingatia masharti ya leseni.

Nauli iliyopangwa kati ya Machinga Complex – vituo vya Mpalasingi, mwanzo wa daraja, getini darajani, JKT, Polisi Ufundi ni Sh 400. Vilevile kutoka vituo vya Mivinjeni, Bandarini, Keep left na Machinga Complex nauli itakuwa Sh 450.

Aidha, imeelezwa kuwa nauli itakuwa Sh 400 kwa safari za njia ya Kigamboni -Temeke kwa vituo vya Mpalasingi, Mwanzo wa daraja, Getini darajani, Uhasibu, Azizi Ally na Temeke.

Kwa njia ya Kigamboni –Mbagala Rangi tatu, nauli itakuwa Sh 400 kwa vituo vya Mpalasingi, mwanzo wa daraja, getini darajani, Azizi Ally, Mtongani . Nauli ya Sh 450 itatozwa kwa vituo vya Msikitini Kizinga, Misheni, Sabasaba kwa Mpili, Kipati, Kizuiani, Zakhem na Mbagala Rangi Tatu. xx

Sambaza Makala hii: Share on Facebook5Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By