Habarika | "SIZONJE YA MRISHO MPOTO ILIMTABIRI RAIS MAGUFULI" ASEMA NAPE
layout-wrap boxed
Tuesday, May 22, 2018

“SIZONJE YA MRISHO MPOTO ILIMTABIRI RAIS MAGUFULI” ASEMA NAPE

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema wimbo wa Sizonje ulioimbwa na msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto ulitabiri utendaji kazi wa rais John Magufuli.

Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa Video ya wimbo huo jijini Dar es salaam, Nape alisema wimbo huo wa Mpoto unaonyesha njia ya Magufuli anavyotakiwa kufanya katika uongozi wake.

Alisema wimbo wa Sizonje umeimbwa kwa umaridadi mkubwa na umetungwa kwa maneno yenye maana na tija kubwa kwa viongozi, Katika uzinduzi huo ambao uliambatana na kuwapa tuzo wasanii waliofanya vizuri kwenye mtihani wa kidato cha nne hususani somo la Kiswahili, pia Nape ameahidi kumsaidia mwanafunzi aliyekuwa wa mwisho kitaifa katika mtihani huo hadi ahakikishe ndoto zake zinatimia licha ya kufeli.

Kwa upande wake Mpoto alisema ameamua kufanya tukio hilo la kauli mbiu ya kufeli shule sio kufeli maisha ili kila mwanafunzi ajue kuwa bado ana nafasi ya kutengeneza maisha yake.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook8Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By