Habarika | SHOO YA BEYONCE YAZUA UTATA.
layout-wrap boxed
Tuesday, May 22, 2018

SHOO YA BEYONCE YAZUA UTATA.

Meya wa zamani wa jiji la New York nchini Marekani, Bwana Rudy Giuliani amechukizwa na kitendo cha mwanamuziki Beyonce Knowles kuonyesha ishara ya kisiasa ya “black power” wakati akitumbuiza kwenye fainali za 50 za mchezo maarufu wa American Football wakati wa muda wa mapumziko kwenye dimba la Levi’s huko jijini California.

Meya huyo amesema kwamba Beyonce hakutakiwa kufanya vile kwani pale ni sehemu mahususi kwa ajili ya michezo na sio Hollywood hivyo hakutakiwa kuonyesha ishara ile ya “Black Power” kwani ila lengo la kuwakashifu maofisa wa polisi ambao ni watu wanaowalinda wao na mali zao.

Ishara hiyo ya Black Power ilitumika mwaka 1968 na wanariadha wa Marekani Tommie Smith na John Carlos wakati wa sherehe za ugawaji tuzo katika michuano ya Olimpiki jijini Mexico City ikiwa ni ishara ya kudai usawa na  kupinga unyanyasaji wa watu weusi nchini Marekani ambao ulikuwa ukifanywa na maofisa wa polisi kwa amri ya serikali ya watu weupe.

” Tunachotakiwa kuwa tunafanya katika jamii zenye mchanganyiko wa watu weusi na weupe na jamii zote kwa ujumla ni kuwaheshimu polisi kwasababu wanajitolea maisha yao kwa ajili yetu, sijapendezwa na kitendo cha Beyonce kutumia shoo yake  kuonyesha ishara ambazo zinaleta uchochezi hasahasa ikiwa ni kejeli kwa jeshi la polisi”. Alisema Rudy Giulian.

beyonce3

Katika shoo hiyo ambayo Beyonce alitumbuiza kwa wimbo wake maarufu wa “Formation” ambao Giulian aliuita ni wimbo wenye uchochezi wa kisiasa ndani yake, wacheza shoo wa Beyonce walivaa nguo nyeusi ambazo ni ishara ya wanaharakati weusi “black panthers” ambacho kilikuwa ni chama cha watu weusi kilichoundwa kupigania haki za watu hao dhidi ya unyanyasaji wa watu weupe nchini humo miaka 50 iliyopita na kumfanya meya huyo kumkosoa Beyonce hususani pale yeye na kundi lake waliponyanyua kiganja juu kilichokunjwa kwa ishara ya ngumi ambacho kilitumika miaka ya nyuma kuashiria umoja wa watu weusi yaani “black power”.

 

Sambaza Makala hii: Share on Facebook11Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By