Habarika | SERIKALI YASHUSHA BEI YA SUKARI HADI  SH 1,800/= KWA KILO
layout-wrap boxed
Tuesday, May 22, 2018

SERIKALI YASHUSHA BEI YA SUKARI HADI  SH 1,800/= KWA KILO

Bodi ya sukari Tanzania imeshusha bei ya Sukari kwa kutangaza bei elekezi inayoonesha bidhaa hiyo kuanzia sasa inauzwa Sh 1,800 kwa kilo nchini kote.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa bodi, Henry Simwanza aliwataka wafanyabiashara kuhakikisha kuwa sukari inaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa wananchi bila kuihodhi.

Awali juzi, alipozungumza na waandishi wa habari, Simwanza alisema bei elekezi ya sukari ilikuwa Sh 2,000 kwa Dar es Salaam na miji jirani. Kwa upande wa mikoa iliyo pembezoni, bei elekezi iwe 2,200

Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema juzi wakati akisisitiza bei elekezi hiyo (ya awali), kulikuwa na kikao kingine kikiendelea kujadili suala la sukari, ambacho ndicho kilifikia uamuzi wa bei ya Sh 1,800 baada ya kujiridhisha.

“Kuhodhi bidhaa ni kuhujumu uchumi wanchi, sukari ni bidhaa nyeti inayohitajika sana. Tunawataka wafanyabiashara wote watii agizo hili” Alisema Simwanza

Alisema maofisa wa bodi ya sukari Tanzania, kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za serikali, hususani maofisa biashara wa mikoa na wilaya watafuatilia na kusimamia utekelezaji wa agizo hilo la bei elekezi.

“Serikali ikisema kitu ni amri. Niseme tu hatutasita kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa wale watakaobainika kupandisha bei au kuhodhi bidhaa hiyo”, alisema Simwanza

Juzi Simwanza akizungumza na waandishi wa habari alisema upatikanaji wa sukari nchini ni wa kuridhisha na ipo akiba ya kutosheleza nchi nzima.

 

Sambaza Makala hii: Share on Facebook1Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By