Habarika | SERIKALI YAKANUSHA TUHUMA ZA KUWAPENDELEA WANAVYUO AMBAO NI WANACHAMA WA CCM
layout-wrap boxed
Sunday, February 25, 2018

SERIKALI YAKANUSHA TUHUMA ZA KUWAPENDELEA WANAVYUO AMBAO NI WANACHAMA WA CCM

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali haijatoa maelekezo yoyote ya siasa yanayohusiana na upendeleo vyuoni

Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tarime Mjini kupitia Chadema Esther Matiko aliyeuliza swali kwamba serikali imetoa maagizo ya wanafunzi wanaounga mkono CCM kupendelewa vyuoni hasa Chuo Kikuu cha Dodoma.

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amesema kwamba si kweli kwamba kuna maelekezo yoyote yametolewa na serikali kuwanyanyasa wanafunzi ambao hawaiungi mkono CCM na hata hivyo kila mtu ana haki ya kujiunga na chama chochote mradi afuate sheria za mahali husika.

”Mtumishi yeyote au mwanafunzi ana haki ya kujiunga na chama chochote lakini lazima afuate sheria , Tanzania hii ni yetu sote na kila mmoja ana uhuru wa kujiunga na chama chochote anachotaka na serikali itaendelea kuwahudumia wananchi wote bila kujali vyama vyao”- Amesema Waziri Mkuu.

Aidha Waziri Mkuu amesisitiza wanafunzi kuheshimu sheria za vyuo vyao vya kutojihusisha na siasa wakati wa masomo ili kujiepusha na migongano isiyokuwa ya lazima.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaendelea na vikao vyake mjini Dodoma ambapo jambo kubwa linalosubiriwa ni kupitiswa kwa bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016 & 2017.

-EATV

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like


Warning: file_get_contents(http://graph.facebook.com/?ids=http://habarika.com/serikali-yakanusha-tuhuma-za-kuwapendelea-wanavyuo-amba0-ni-wanachama-wa-ccm/): failed to open stream: HTTP request failed! HTTP/1.1 403 Forbidden in /home/habarika/public_html/wp-content/themes/habarika/elements/element.php on line 80
0 comments

By