Habarika | SERIKALI YAITAKA NHC KUJENGA NYUMBA ZA BEI NAFUU.
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

SERIKALI YAITAKA NHC KUJENGA NYUMBA ZA BEI NAFUU.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, ndugu William Lukuvi (mb) ameliagiza Shirika la Nyumbala Taifa NHC kujenga nyumba za gharama nafuu utakaokuwa na ukweli wa unafuu huo.

Hayo yameelezwa alipotembelea ofisi za shirika hilo mkoani Mbeya ambazo pia huhudumia mkoa wa Njombe. Lukuvi alisema

“Acheni kuilalamikia serikali kwa kuchukua fedha za ongezeko la thamani (VAT) kwamba ndio inayoongeza gharama za ujenzi.”

Lukuvi alilitaka shirika hilo kufanya utafiti wa kina juu ya namna gani linaweza kujenga nyumba za gharama nafuu kiukwelikweli ambazo zitaweza kujengwa mijini na kwenye miji midogo midogo vijijini.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By