Habarika | SERIKALI YA ZANZIBAR YAJIANDAA KUANZA KUCHUKUA MAAMUZI MAGUMU
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

SERIKALI YA ZANZIBAR YAJIANDAA KUANZA KUCHUKUA MAAMUZI MAGUMU

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amesema Serikali italazimika kuchukuwa uamuzi mgumu katika kukabiliana na watu waliojenga nyumba bila ya vibali na bila uzingatiaji wa taratibu za ardhi.

Alisema uamuzi huo utahusu zaidi maeneo yaliyowekwa kwa ajili ya miradi ya kijamii, vianzio vya maji pamoja na mitaro ya kupitishia maji ya mvua.

Alitoa agizo hilo jana kwa masheha wote wa wilaya mbili za Magharibi “A” na “ B” akiwataka kuanza kuorodhesha nyumba zote zilizojengwa bila ya kibali na katika maeneo yasiyostahiki.

“Tunakusudia kubomoa majengo yote yaliyojengwa bila ya kibali na kwenye maeneo ya njia za maji, ikiwa ni mwanzo wa uamuzi mgumu utakaochukuliwa na Serikali,” alisema Balozi Seif.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook1Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By