Habarika | SAKATA LA MSHAHARA WA RAIS, KATIBU MKUU UTUMISHI AFUNGUKA
layout-wrap boxed
Sunday, February 25, 2018

SAKATA LA MSHAHARA WA RAIS, KATIBU MKUU UTUMISHI AFUNGUKA

Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) imefafanua kuhusu mshahara wa Rais John Magufuli ikisema  kuwa mishahara ya watumishi wa umma hupangwa katika bajeti, hivyo mshahara wa Rais ni ule ulioidhinishwa katika Bajeti ya mwaka 2015/16.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, laurian Ndumbalo, bajeti ya mishahara yote ya watumishi wa umma na viongozi wa umma hupangwa kila wakati pale bajeti inapoandaliwa na kuidhinishwa na kwamba Rais mpya hakutengenezewa mshahara mpya

“Wizara yetu ndiyo yenye dhamana ya mishahara ya watumishi wa umma na viongozi wa umma, na hii huandaliwa kila mwanzo wa mwaka kabla ya kuanza kwa mwaka mpya wa fedha. Kwa hiyo mwaka 2015/16 fedha zake ziliidhinishwa Juni mwaka jana na kuanza kutumika Julai”, alisema Dk Ndumbaro.

“Kwa hiyo bajeti hiyo iliidhinishwa na viongozi wote, Rais, Makamu wa Rais, wabunge na watumishi wote wa umma. Hivyo, mshahara wa Rais, kwa mantiki hiyo, Rais Kikwete ndio huo ambao unatumiwa na Rais John Magufuli. Kama mshahara, hakuna tofauti, hakuna mabadiliko, kiwango ni kilele. Rais mpya hakutengenezewa mshahara mpya” alifafanua

Katibu mkuu huyo wa Utumishi na Utawala bora. Kumekuwapo na taarifa mbalimbali katika vyombo vya habari kuhusu mshahara wa Rais na hivi karibuni, baadhi ya vyombo vya habari vilidai kuwa Rais mstaafu Kikwete alikuwa analipwa Sh milioni 34

Aidha, Rais Magufuli alikaririwa hivi karibuni akiwa nyumbani kwake Chato mkoani Kagera akisema kuwa analipwa mshahara wa Sh milioni 9.5

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone


Warning: file_get_contents(http://graph.facebook.com/?ids=http://habarika.com/sakata-la-mshahara-wa-rais-katibu-mkuu-utumishi-afunguka/): failed to open stream: HTTP request failed! HTTP/1.1 403 Forbidden in /home/habarika/public_html/wp-content/themes/habarika/elements/element.php on line 80
0 comments

By