Habarika | SAFARI YA KWANZA YA MAGUFULI NJE YA NCHI YAANGUKIA RWANDA
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

SAFARI YA KWANZA YA MAGUFULI NJE YA NCHI YAANGUKIA RWANDA

Rais Magufuli leo atafanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi baada ya kukaa nchini siku zote tangu ashike madaraka ya kuiongoza Tanzania Novemba 5 mwaka jana kwa kuzuru Rwanda

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya nje Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Rais Maguful atatoka kwa mara ya kwanza nje ya anga la Tanzania baada ya siku 1515 kwa mwaliko wa Rais paul kagame wa Rwanda

Taarifa hiyo ilisema Dk Magufuli atakuwa na ziara ya siku mbili ya kikazi katika nchi hiyo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na ambayo pia ni mshirika wa karibu wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wakati wa ziara hiyo, Rais Magufuli na mwenyeji wake Rais Kagame wanatariwa kuzindua daraja la kimataifa la Rusumo pamoja na Kituo cha Pamoja cha Forodha (OSBP) ambacho ni kituo muhimu katika kurahisisha mwingiliano kati ya nchi hizo mbili, lakini pia kitaboresha matumizi uhusiano na matumizi ya Rwanda katika Bandari ya Dar es Salaam

Baada ya sherehe za Uzinduzi, viongozi hao wawili watakwenda jijini Kigali ambako watafanya mazungumzo kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili na pamoja wataweka shada la maua kwenye kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari mjini Kigali ikiwa ni kukumbuka mauaji ya Kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994

Akiwa mwenyekiti wa EAC, ziara hii ya kwanza nje ya nchi ya Rais Magufuli akiifanya katika ukanda huo, na pia inaonesha msimamo wake wa kisiasa katika kuimarisha mchakato wa utengamano na mahusiano kati ya nchi wanachama wa EAC.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook2Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By