Habarika | RAILA ODINGA: NAJUA MAGUFULI ANA MAONO YA KUWASAIDIA WATANZANIA
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

RAILA ODINGA: NAJUA MAGUFULI ANA MAONO YA KUWASAIDIA WATANZANIA

Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Raila Odinga amerejea  nchini Kenya baada ya kumaliza mapumziko yake ya siku tatu Lubambangwe katika kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato mkoani Geita alikomtembelea Rais Magufuli aliyepo mapumzikoni.

Akizungumza kwenye uwanja wa michezo kwa Shule ya Sekondari ya Chato kabla ya kuruka kwa helikopta, Raila alimshukuru rafiki yake Rais Magufuli kwa kumpokea na pia aliwashukuru wananchi wa Chato kwa ukarimu wao kwa wageni.

Pia alisema ana imani kuwa Rais Magufuli ataisaidia Tanzania kukabiliana na changamoto mbalimbali, ikiwemo umasikini unaowakabili wananchi wake.

“Lakini mimi najua yeye mwenyewe ana maono, anaona mbele na anajua yale ambayo yanatakiwa yafanyike ili Tanzania iinuke, itoke katika hali ya ufukara na kuwa katika hali ya maendeleo zaidi”, alisema Raila

Raila na mkewe, Mama Ida Odinga waliwasili Chato, Jumamosi iliyopita kwa mapumziko na kuisalimia familia ya Rais Magufuli ambayo ni familia rafiki

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ameahidi kutoa madawati na vitabu kwa wanafunzi wa shule tatu za msingi zilizopo Chato, ambao walijitokeza Uwanja wa Sekondari wa Chato wakati Rais Magufuli akimuaga mgeni wake Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Raia Odinga.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By