Habarika | PROF. MBARAWA ATOA DARASA KWA SHIRIKA LA POSTA NA TTCL
layout-wrap boxed
Friday, April 27, 2018

PROF. MBARAWA ATOA DARASA KWA SHIRIKA LA POSTA NA TTCL

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame  Mbarawa amewataka watendaji wa Shirika la Posta Tanzania na   Kampuni ya simu ya (TTCL) kufanya kazi kwa weledi na mtazamo  wa kibiashara  ili kuyaongezea mapato mashirika hayo na hivyo  kuendana na  mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanaoyotokea nchini.

Akizungumza na wafanyakazi wa TTCL na POSTA mkoani Mwanza Prof. Mbarawa amesema kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano duniani, biashara ya simu na posta hivi sasa zina ushindani mkubwa unaohitaji mtazamo mpana wa kibiashara ili kukidhi mahitaji ya soko.

“Serikali inajitahidi kuisaidia TTCL na POSTA hivyo wekezeni vizuri kwenye data na uharaka wa utoaji huduma ili muweze kushindana kwenye soko na kukuza uchumi wa taasisi hizi muhimu kwa usitawi wa nchi”, amesema Prof Mbarawa.

Prof. Mbarawa amezitaka menejimenti za POSTA na TTCL kufanya kazi kwa uwazi na uadilifu ili malengo na mikakati ya taasisi hizo yafahamike kwa wafanyakazi wote na kuwezesha kujipima kama wanafikia malengo yaliyokusudiwa.

“Hakikisheni wafanyakazi wote wanaelewa malengo na mikakati ya tasisi zenu ili kazi ya kuyatekeleza ifanywe kwa umoja na ushirikiano”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

CHANZO: TUAMBIE

Sambaza Makala hii: Share on Facebook4Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By