Habarika | PANYA WA KUTEGUA MABOMU WALIOGUNDULIWA SUA WAWA KIVUTIO DUNIANI
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

PANYA WA KUTEGUA MABOMU WALIOGUNDULIWA SUA WAWA KIVUTIO DUNIANI

Soko la panya waliogunduliwa na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) wenye uwezo wa kutegua mabomu na kubaini ugonjwa wa kifua kikuu, limezidi kuongezeka baada ya nchi nyingi kuwahitaji.

Nchi za Cambodia, Vietnam, Thailand na nyinginezo zilizopitia katika vita zimeonesha kufanikiwa na panya hao na sasa wanahitaji wengine zaidi ya 10 ili kusambaza katika maeneo mbalimbali ya nchi hizo.

Pia nchini Ethiopia wamehitaji panya zaidi ya 10 kwa ajili ya kubaini ugonjwa wa kifua kikuu kutokana na panya hao kuwa na uwezo wa kubaini mgonjwa ambaye ugonjwa huo haujaonekana kwa vipimo vya kawaida.

Mtafiti wa Kituo cha Utafiti na Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibifu wa SUA, Dk Georgies Mgode alisema awali panya wa kutegua mabomu waliishapelekwa katika nchi za Msumbiji, Angola na 16 Cambodia na kuonesha mafanikio makubwa sana.

Alisema kwa sasa wanaomba vibali katika Wizara ya Maliasili na Utalii kupeleka panya hao wanaohitajika katika mwisho wa mwaka huu au mwanzoni mwa mwakani.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook5Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By