Habarika | NGULI WA SOKA, JOHAN CRUYFF AFARIKI DUNIA KWA KANSA YA MAPAFU
layout-wrap boxed
Friday, April 27, 2018

NGULI WA SOKA, JOHAN CRUYFF AFARIKI DUNIA KWA KANSA YA MAPAFU

Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi na klabu ya Barcelona, Johan Cruyff amefariki dunia kwa ugonjwa wa kansa akiwa na miaka 68

Cruyff amefariki leo huko Barcelona nchini Hispania akiwa amezungukwa na familia baada ya kusumbuliwa na kansa ya mapafu.

Cruyff alijitokeza kuwa mmoja wa wachezaji mahiri duniani mwanzoni mwa miaka ya 1970 alipoisaidia klabu yakke ya Ajax Amsterdam kushinda mataji matatu ya Ulaya mfululizo kuanzia mwaka 1971 hadi 1973 na akatajwa uwa mchezaji bora wa mwaka wa bara la Ulaya kwa miaka ya 1971, 1973 na 1974.

Alijiunga na Barcelona kwa ada ya rekodi ya dunia kwa kipindi hicho ya dola milioni 2.0 na ndipo hapohapo nyota huyo alifanikiwa kuwaongoza Barca kutwaa taji la kwanza  la La Liga baada ya miaka 15, mwaka 1974. Lakini pia mwaka huohuo wa 1974, Cruyff aliisaidia timu yake ya taifa ya Uholanzi kufika fainali ya kombe la dunia.

Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu Johan Cruyff. Amen

Sambaza Makala hii: Share on Facebook3Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By