Habarika | MWISHO SAA SITA MCHANA WA LEO KWA RAIS WA GAMBIA KUACHIA MADARAKA LASIVYO ATATOLEWA KINGUVU
layout-wrap boxed
Tuesday, May 22, 2018

MWISHO SAA SITA MCHANA WA LEO KWA RAIS WA GAMBIA KUACHIA MADARAKA LASIVYO ATATOLEWA KINGUVU

Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi wamempa Yahya Jammeh fursa ya mwisho kuachia madaraka, huku wanajeshi wa Senegal wakiingia nchini Gambia.

Bw Jammeh amepewa hadi saa sita mchana Ijumaa kuachia madaraka la sivyo aondolewe kwa nguvu na wanajeshi wa nchi za Afrika Magharibi wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambapo wanajeshi hao wametakiwa kusubiri hadi muda wa fursa ya mwisho aliyopewa utakapomalizika

Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) inamuunga mkono Adama Barrow, ambaye aliapishwa kuwa rais mpya wa Gambia katika ubalozi wa nchini hiyo nchini Senegal.

Juhudi za mwisho za kumshawishi Bw Jammeh kuondoka kwa hiari, ambazo zinaongozwa na Rais wa Guinea Alpha Conde, zinatarajiwa kufanyika Ijumaa asubuhi.

Mwenyekiti wa tume ya Ecowas, Marcel Alain de Souza, alisema iwapo mkutano huo utakaoongozwa na Bw Conde hautafaulu, basi hatua ya kijeshi itafuata.

“Iwapo kufikia saa sita mchana, yeye (Bw Jammeh) hatakubali kuondoka Gambia chini ya Rais Conde, tutaingilia kijeshi,” amesema.

Wanajeshi kutoka Senegal na nchi nyingine za Afrika Magharibi waliingia Gambia baada ya muda wa nafasi za mwisho alizopewa Bw Jammeh kuondoka kumalizika.

Bw Jammeh, ambaye bado yupo nchini Senegal amesema hatarejea mji mkuu wa Gambia, Banjul, hadi operesheni ya kijeshi imalizike.

Hatua ya Ecowas kutaka kumtoa kwa nguvu Jammeh inaungwa mkono na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 15, ingawa baraza hilo lilisisitiza kwamba suluhu ya amani inafaa kutopewa kipaumbele.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook8Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By