Habarika | MTUHUMIWA WA MADAWA YA KULEVYA NCHINI RAIA WA IRAN AFARIKI DUNIA
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

MTUHUMIWA WA MADAWA YA KULEVYA NCHINI RAIA WA IRAN AFARIKI DUNIA

Mshtakiwa Ayoub Mohamed anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na kuingiza nchini dawa za kulevya zenye thamani ya Sh bilioni 9.02 amefarikia dunia.

Wakili wa serikali Mwanaamina Kombakono alidai hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati kesi hiyo ilipotajwa mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu, Waliarwande Lema

Hata hivyo wakili huyo hakueleza sababu ya kifo cha mshtakiwa huyo ambapo aliomba tarehe nyingine ya kutajwa. Hakimu aliahirisha  kesi hadi Aprili 4 mwaka huu. Mbali na Mohamed ambaye alikuwa nahodha na raia wa  Iran, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Buksh Mohamed, Fahiz Dauda, Khalid Ally, Abdul Somad, Saeed Sahury, Bashir Afraz, Morad Gwaram na Hazir Azad, wote raia wa Iran

Wengine ni Rahim Baksh na Abdul Bakashi kutoka Pakistan ambao wote ni wavuvi wakikamatwa kwenye Bahari ya Tanzania

Inadaiwa Februaari 4, 2014, washtakiwa hao walikamatwa wakiwa na kilo 200.5 za dawa za kulevya aina ya heroine, zenye thamani ta Sh bilioni 9.2 wakizisafirisha kwa  njia ya bahari

-HABARI LEO

Sambaza Makala hii: Share on Facebook2Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By