Habarika | MTOTO WA KIZZA BESIGYE AWANIA URAIS CHUO KIKUU CHA OXFORD
layout-wrap boxed
Tuesday, December 12, 2017

MTOTO WA KIZZA BESIGYE AWANIA URAIS CHUO KIKUU CHA OXFORD

besi

Mtoto wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye ni miongoni mwa wanafunzi waliojitokeza kuwania urais katika chama cha mijadala chuo cha Oxford.

Anselm Besigye ametengeneza video fupi (Bonyeza hapo nyuma kutazama) ya kuwaomba wanafunzi wenzake wampigie kura.

Anasimulia mambo ambayo amefanyia chama hicho na uzoefu wake katika mijadala.

Mwisho wa video mamake Anselam Winnie Besigye, anaonekana na kusema “huna budi kushinda uchaguzi huu, nimekusaidia sana!”.

Babake Anslem, Dkt Kizza Besigye, amewania urais mara nne dhidi ya kiongozi wa muda mrefu wa Uganda Yoweri Museveni bila mafanikio.

Anazuiliwa kwake nyumbani na maafisa wa usalama tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu tarehe 20 Februari.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like


Warning: file_get_contents(http://graph.facebook.com/?ids=http://habarika.com/mtoto-wa-besigye-awani-urais-chuo-kikuu-cha-oxford/): failed to open stream: HTTP request failed! HTTP/1.1 403 Forbidden in /home/habarika/public_html/wp-content/themes/habarika/elements/element.php on line 80
0 comments

By