Habarika | MTANDAO WA ‘KWANZA’ KWA AJILI YA MATANGAZO YOTE YA KIDIGITALI TANZANIA WAZINDULIWA
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

MTANDAO WA ‘KWANZA’ KWA AJILI YA MATANGAZO YOTE YA KIDIGITALI TANZANIA WAZINDULIWA

Kampuni ya matangazo ya kidigitali ya Smartcodes imezindua rasmi mtandao ujulikanao kama “Kwanza” ambalo ni jukwaa mahsusi kwa ajili ya kujumuisha matangazo yote ya kidigitali ndani ya mtandao mmoja Tanzania.

Jukwaa hilo la kitaalamu la ‘Kwanza’ ambalo ni la kwanza kwa Tanzania litawezesha bidhaa na watangazaji wa bidhaa hizo kuwafikia mamilioni ya watumiaji kupitia simu zao za mikononi, tovuti na kifaa chochote kinachotumia mtandao (internet)

kwanza2

 Akiuzungumzia mtandao huo, Edwin Bruno ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Smart Codes amesema kuwa mtandao huo una lengo la kutatua matatizo ya kuwafikia watumiaji walengwa wa bidhaa kupitia simu zao za mikononi kitu ambacho kimekuwa ni changamoto kubwa katika taaluma ya masoko kwa sasa

“Kwa nchi kama ya Tanzania yenye watumiaji wa mtandao zaidi ya milioni 17.26, changamoto iliyozoeleka kwa wanataaluma wa masoko limekuwa ni kuwaelewa na kuwatambua watumiaji kupitia vifaa vyao, jinsi ya kuwalenga na mwisho upimaji sahihi wa matangazo yaliyonunuliwa”, Alisema Edwin Bruno, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Smart Codes.

“Kwanza inafanya bidhaa kuwalenga watumiaji wake kulingana na eneo husika kwa kutumia kifaa tu au mfumo wa uendeshaji kwa muda muafaka, siku ndani ya wiki au mwezi. Kwa mfano, kama biashara yako ipo Dar, kwanini upoteze matangazo yako ya thamani kwa watumiaji wa Mtwara? Alifafanua Edwin Bruno

Naye Herman Mkamba ambaye ni Mnunuzi wa Matangazo ya Mitandaoni wa Kampuni hiyo ya Smart Codes ameongeza kuwa app hiyo ya Kwanza itakuwa ikitoa taarifa sahihi kwa kampeni za matangazo, kiasi kilichotumika na matangazo yanayofanya vyema.

“Taarifa zote zitakuwa zikipatikana kwenye dashibodi ya mtangazaji mwenyewe na kwenye app ya Android ya Kwanza. Ukiwa na app hii utapata muhtasari na takwimu za kina ikiwa ni pamoja na kutengeneza na kusimamisha kampeni, kuweza kupata rekodi ya matumizi na usawa, kuona wapi na matangazo gani yanafanya vizuri ambapo hayo yote utakuwa ukiyapata kwa kutumia ncha za vidole vyako, popote na muda wowote”, alimalizia Herman Mkamba.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook18Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By