Habarika | RIO 2016: MMISRI AONDOLEWA MASHINDANONI KWA KUKATAA KUPEANA MIKONO NA MPINZANIWE KUTOKA ISRAEL
layout-wrap boxed
Friday, April 27, 2018

RIO 2016: MMISRI AONDOLEWA MASHINDANONI KWA KUKATAA KUPEANA MIKONO NA MPINZANIWE KUTOKA ISRAEL

Mchezaji wa Judo kutoka Misri Islam El Shehaby amerudishwa nyumbani kutoka katika michezo ya Olimpiki baada ya kukataa kusalimiana kwa mkono na mpinzani wake Sasson kutoka Israel baada ya pigano lao.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alipewa adhabu hiyo na kamati ya michezo ya Olimpiki baada ya kupoteza katika raundi ya kwanza siku ya Ijumaa.

Kamati ya Olimpiki imesema kuwa tabia yake inaenda kinyume na sera ya urafiki iliopo katika maadili ya michezo hiyo ambapo kamati ya Olimpiki ya Misri ilimshtumu El Shehaby na kumrudisha nyumbani.

El Shehaby baadaye alizomewa na mashabiki waliokuwa wamejaa katika ukumbi wa mchezo huo na alitakiwa kurudi katika ukumbi huo ili kutoa heshima kwa mpinzani wake kwa kuwa ni kinyume na sheria za mchezo huo.

Sasson hatahivyo alibaini kwamba makocha wake walimuonya kwamba El Shehaby huenda asimsalimie kwa kushikana mikono.

Inadaiwa kwamba raia huyo wa Misri alikuwa ameshinikizwa na baadhi ya mashabiki wake kutoka nyumbani kutoshiriki katika pigano hilo.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By