Habarika | MILIONI 50 ZA RAIS MAGUFULI VIJIJINI KUSIMAMIWA NA WAKUU WA MIKOA
layout-wrap boxed
Saturday, March 24, 2018

MILIONI 50 ZA RAIS MAGUFULI VIJIJINI KUSIMAMIWA NA WAKUU WA MIKOA

Kazi ya kusimamia Sh milioni 50 zilizopangwa kutolewa kwa kila kijiji kwa ajili ya kukabili umasikini wamepewa wakuu wa mikoa

Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu alisema jana kwamba Serikali imejiandaa kutimiza ahadi ya kutoa fedha hizo na utekelezaji wake, utaanza katika bajeti ijayo ya mwaka 2016/2017

Akizungumza baada ya wakuu hao wa mikoa kutia saini kiapo cha utii, Ikulu Dar es Salaam, Samia alisema fedha hizo lengo lake ni kupunguza umasikini kuanzia ngazi ya chini

“Najua kuna taasisi mbalimbali zimekuwa zikiwafikia na kuwasaidia wananchi katika hili ukiwemo mfuko wa Maendeleo ya Jamii  (TASAF) na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za  wanyonge Tanzania (Mkarabita) lakini bado kuna kazi kubwa ya kuwafikia wananchi masikini”, alisema Mama Samia

Alisema fedha hizo zimeanza kuingizwa kwenye bajeti hiyo na zinategemea kusambazwa katika vijiji vyote mwanzoni mwa utekelezji wa bajeti hiyo

“Napenda niwafikishie maagizo ya Rais Magufuli kwenu kuwa fedha hizi zinakuja kwenu, zisimamieni ili zifanye kazi iliyokusudiwa”, alisisitiza

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By