Habarika | Michezo
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

Michezo

Mchezaji wa Judo kutoka Misri Islam El Shehaby amerudishwa nyumbani kutoka katika michezo ya Olimpiki baada ya kukataa kusalimiana kwa mkono na mpinzani wake Sasson kutoka Israel baada ya pigano lao.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alipewa adhabu hiyo na kamati ya michezo ya Olimpiki baada ya kupoteza katika raundi ya kwanza siku ya Ijumaa.

Kamati ya Olimpiki imesema kuwa tabia yake inaenda kinyume na sera ya urafiki iliopo katika maadili ya michezo hiyo ambapo kamati ya Olimpiki ya Misri ilimshtumu El Shehaby na kumrudisha nyumbani.

El Shehaby baadaye alizomewa na mashabiki waliokuwa wamejaa katika ukumbi wa mchezo huo na alitakiwa kurudi katika ukumbi huo ili kutoa heshima kwa mpinzani wake kwa kuwa ni kinyume na sheria za mchezo huo.

Sasson hatahivyo alibaini kwamba makocha wake walimuonya kwamba El Shehaby huenda asimsalimie kwa kushikana mikono.

Inadaiwa kwamba raia huyo wa Misri alikuwa ameshinikizwa na baadhi ya mashabiki wake kutoka nyumbani kutoshiriki katika pigano hilo.

Muogeleaji wa Kichina He Zi alikuwa amepokea medali yake ya fedha katika mchezo wa Springboard katika michezo ya Rio ya Olimpiki siku ya jumapili.
Wachina wachumbiana Rio de janeiro

Lakini alipata zawadi nyingine wakati mpenzi wake Qin Kai mbele ya matangazo ya runinga yaliokuwa yakipeperushwa duniani kupiga goti moja na kumuomba awe mkewe wa ndoa na kwa bahati nzuri, Qin ambaye yeye mwenyewe alishinda medali ya shaba alilikubali ombi hilo

Wachina wachumbiana Rio de janeiro

”Tumekuwa wapenzi kwa miaka sita, lakini sikudhani kwamba atanichumbia leo”,alisema.

Amesema kuwa :Vitu vingi vilileta ahadi nyingi, lakini kitu kilichonigusa zaidi ni kwamba huyu ndio mtu ninayeweza kumuamini kwa maisha yangu yote.

Wachina wachumbiana Rio de janeiro

Watazamaji wamesema kuwa kisa hicho cha kipekee kilitawala sherehe za kutoa medali katika michezo hiyo.

Wachina wachumbiana Rio de janeiro

Chanzo: BBC Swahili

Picha hii ya pamoja ya wanamichezo hawa wawili kutoka nchi hizi hasimu imekamilisha dhana ya michezo ni amani na pindi watu wakusanyikapo kwenye michezo basi huwafanya kusahau kwa muda tofauti zao za kisiasa.

Wanamichezo wa mazoezi ya viungo kutoka Korea Kusini na Kaskazini, ambao wanashiriki Michezo ya Olimpiki Rio 2016, wameuonesha ulimwengu ishara ya umoja, kwa kupiga selfie pamoja.

Lee Eun-ju wa Korea Kusini na Hong Un-jong wa Korea Kaskazini walipiga picha wakiwa wametabasamu wakati wa mazoezi kabla ya kuanza kwa michezo hiyo.

smile

Picha za wanawake hao wawili zimesifiwa sana kwa kuashiria moyo wa Olimpiki wa kuwaleta watu pamoja.

Korea Kaskazini na Korea ni nchi zenye uhasama mkubwa kidiplomasia licha ya nchi hizo mbili kuwa na utamaduni unaofanana lakini wamekuwa mahasimu  baada ya vita vya pili vya dunia huku mwaka 1950 Korea Kaskazini waliivamia Korea Kusini kwa msaada wa Marekani ambapo China aliingilia vita hivyo kumsaidia Korea Kaskazini hali iliyoleta usawa katika vita hiyo.

Vita baina yao ilimalizika mwaka 1953 hali iliyopelekea kuwepo kwa mipaka baina ya Kaskazini na Kusini kitu ambacho kimezorotesha uhusiano baina yao huku kitendo cha Korea kaskazini kufanya majaribio ya makombora kwenye upande wa bahari wa Korea Kusini kimeendelea kuongeza uhasama baina yao kwa kile kinachosemekana kuwa Korea Kaskazini wanaitisha Korea Kusini ambayo ni mshirika mkubwa wa Marekani.

Picha hii ya pamoja ya wanamichezo hawa wawili kutoka nchi hizi hasimu imekamilisha dhana ya michezo ni amani na pindi watu wakusanyikapo kwenye michezo basi huwafanya kusahau kwa muda tofautizao za kisiasa.

 

 

Mwenge wa Olimpiki umefika katika mji wa Rio de Janeiro kwa kutumia usafiri wa boti baada ya ziara ya muda wa miezi mitatu kuzunguuka miji mikubwa ya Brazil.

Meya wa mji wa Rio, Eduardo Paes, ndiye aliyeubeba mwenge huo wa Olimpiki miongoni mwa watu wachache waliofanikiwa kuushika.

Safari hiyo ya miezi mitatu haikuwa rahisi kwani kuna wakati msafara wa mwenge huo wa Olimpiki ulipokuwa ukipitishwa ulikumbana na waandamanaji wenye hasira kali kuhusiana na suala la gharama kubwa zilizotumika mpaka kuwa wenyeji wa michuano hiyo maarufu ulimwenguni.

Polisi wa kutuliza ghasia iliwalazimu kutumia mabomu ya machozi na pilipili za kupuliza ili kuwatawanya waandamanaji hao wenye hasira .Kwa sasa nchi ya Brazil inapita katika kipindi cha mpito wa hali mbaya ni katika mtego wa anguko kubwa la kiutawala na mgogoro wa kisiasa, na maandamano zaidi yanatarajiwa siku ya ufunguzi wa michuano hiyo ya Olimpiki inayotarajiwa siku ya Ijumaa.

Waandaaji wa michuano hiyo wameonesha masikitiko yao makubwa kutokana na mwitikio mdogo ulooneshwa na wabrazil kwani tiketi zaidi ya milioni moja bado hazijanunuliwa huku sherehe za ufunguzi zimekaribia.

Serikali imeitaka timu ya Tanzania itakayoshiriki Michezo ya 31 ya Olimpiki kuhakikisha inarejea na medali kutoka katika michezo hiyo nchini Brazil.

Michezo hiyo itaanza Ijumaa ya wiki hii hadi Agosti 21 ambapo timu hiyo yenye wachezaji wa riadha (4), kuogelea (2) na judo (1), iliagwa jana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura kwenye Uwanja wa Taifa.

Wambura katika hafla hiyo alisema kuwa anatambua changamoto walizopitia wanamichezo hao wakati wa maandalizi ya kushiriki michezo hiyo mikubwa inayoshirikisha zaidi ya mchezo mmoja duniani.

Pia, naibu waziri huyo aliwapongeza wanamichezo wote waliofuzu na wale wanaoshiriki michezo hiyo kwa nafasi za upendeleo kwa jitihada zao walizofanya wakati wakijiandaa kwa michezo hiyo.

Aliwataka wachezaji hao kupambana ili kupeperusha vizuri bendera ya Tanzania na kutangaza utamaduni wa Tanzania zikiwemo ngoma za asili. Pia aliwapongeza wadhamini mbalimbali, ambapo aliwataka kudhamini na michezo mingine ambayo haipewi kipaumbele.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Elisante ole Gabriel aliwataka Bodi ya Utalii (TTB) kuwapeleka wanamichezo hao katika mbuga za wanyama watakaporejea kutoka Brazil.

Wanariadha wanaounda timu hiyo ni Alphonce Felix, Said Makula, Fabian Joseph na mwanadada pekee katika riadha, Sarah Ramadhani, ambao wote watashiriki marathon.

Waogeleaji ni Magdalena Moshi na Hilal Hemed Hilal wakati mchezaji pekee wa judo ni Andrew Thomas. Makocha watakaoongozana na timu hizo ni Francis John (riadha), Alexander Mwaipasi (kuogelea) na Zaid Hamisi (judo) wakati daktari wa timu ni Nassoro Matuzya.

Waogeleaji na mchezaji huyo wa judo na makocha wao wanaoondoka leo kwa ndege mbili tofauti huku mwanariadha wakike ataondoka Agosti 10 na wale wakiume wataondoka Agosti 15. Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi alisema timu hiyo inaondoka kwa awamu kutokana na ratiba za ndege.

Timu ya judo itaondoka kwa ndege ya Afrika Kusini na kundi la pili litakuwa la kuogelea, ambalo litaondoka saa tisa alasiri na Emirates. Nahodha wa timu hiyo Felix alisema timu ya riadha imejiandaa vizuri baada ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu, ambapo aliahidi kurudi na medali.

Bara la Afrika litatunukiwa nafasi nyengine mbili zaidi iwapo dimba la dunia litaongeza idadi ya mataifa yanayoshiriki hadi 40 kuanzia mwaka 2026 kulingana na rais wa FIFA, Gianni Infantino.

Infantino alipendekeza kuongezwa kwa timu hizo kabla ya kuchaguliwa kwake na shirikisho hilo la soka duniani.

Kwa sasa Afrika ina nafasi tano pekee katika michuano hiyo .

”Pendekezo langu limekuwa timu 40 na iwapo hilo litadhinishwa pendekezo langu ni kulipatia bara la Afrika nafasi mbili zaidi”,alisema Infantino.

Hatahivyo hatua hiyo itaidhinishwa hadi mwaka 2026 huku timu 32 zikiwa tayari zimethibitishwa kushiriki katika kombe la dunia la 2018 nchini Urusi na 2022 nchini Qatar.

Wanariadha wa Urusi hawatashiriki michezo ya Olimpiki ya mwaka huu huko Brazil.

Kauli hiyo imeafikiwa na mahakama ya juu ya michezo ambayo imefutilia mbali rufaa iliyowasilishwa na kamati ya olimpiki ya Urusi ROC ya kuitaka ibatilishe uamuzi wa shirikisho la riadha duniani IAAF ya kuwapiga marufuku wanariadha wake wote wasishiriki michezo ya olimpiki itakayoandaliwa jijini Rio De Jenairo Brazil kuanzia mwezi ujao.

IAAF ilifikia uamuzi huo baada ya kugundulika kuwa serikali ya Urusi ilikuwa na mpango wa chini kwa chini wa kuficha matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku miongoni mwa wanariadha wake.

Kamati ya olimpiki ya Urusi ilikuwa imekata rufaa kwa pamoja na takriban wanariadha 68 ambao hawajawahi kupatikana na hatia ya matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu mwilini.

Baada ya kusikiza pande zote mbili mahakama hiyo ya juu katika riadha CAS imeamua kufutilia mbali rufaa hiyo ambapo kauli hiyo imewadia siku moja tu baada ya uchunguzi huru kubaini kuwa wizara ya michezo ya Urusi, na kamati ya kupambana na matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini ya Urusi zilishiriki udanganyifu ikiwemo kubadilisha mikojo yawanariadha ili vipimo visipatikane na madawa hayo yaliyopigwa marufuku.

Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa IOC imesema itatathmini kwanza hatua za kisheria, kabla ya kufanya uamuzi wowote kuhusu iwapo itaipiga marufuku Urusi kutoshiriki kwenye mashindano ya Olimpiki huko Rio de Janeiro Brazil.

Hatua hii inafuatia ripoti huru kuhusu serikali kuhusika na kuwasaidia wanamichezo wake katika matumizi ya madawa ya kusisimua misuli.

IOC hata hivyo imewafungia maafisa wote wa Urusi kushiriki michuano ya Olimpiki ya Rio, na itawapima tena wanamichezo walioshiriki michuano ya Olimpiki ya majira ya baridi yaliyofanyika Sochi huku tayari wanariadha wa Urusi wakiwa  wamepigwa marufuku na IAAF.

Shirikisho la riadha IAAF limefurahia kauli hiyo ya mahakama ya juu ya michezo ikisema kuwa imesawazisha uwanja wa riadha.

”Kwa hakika tumefurahi kuwa CAS imeunga mkono kauli yetu. Leo kwa hakika sio siku ya kufurahia kwani IAAF haikuja katika michezo kuwazuia wanariadha wasishiriki katika michezo ila nia yetu ni kusawazisha uwanja ili wanariadha wote washindane kwa mizani sawa” alisema rais wa shirikisho la riadha Lord Sebastian Coe.

”Baada ya Rio tutaendelea kuisaidia kamati ya olimpiki ya Urusi ili kuwaruhusu wanariadha wake kurejea katika mashindano ya kimataifa.” aliongezea Coe.

Licha ya uamuzi huo wa CAS, wanariadha wachache wa urusi ambao watakubali kushiriki chini ya bendera ya kamati ya olimpiki wataruhusiwa kushiriki ila lazima wapitie vipimo za ziada ilikuthibitisha kuwa ni wasafi.

Shirika la afya duniani linasema mikusanyiko mikubwa wakati wa kipindi cha michuano ya Olimpiki nchini Brazil haina maana kwamba washiriki wako hatarini kuambukizwa virusi vya zika.

Kamati ya dharura ya WHO juu ya ugonjwa wa ZIKA ilikutana Jumanne ya jana ili kuangalia uwezekano wa hatari katika mikusanyiko mikubwa ya watu katika miji na nchi iliyo na mlipuko wa ZIKA ikiwa ni pamoja na Rio De Janeiro.

Kamati hiyo ilieleza hatari ya mtu mmoja mmoja katika maeneo ya maambukizo iko sawa bila kujali kuna mkusanyiko au la na inaweza kupungua kwa kufuata masharti ya afya.

Idara hiyo ya umoja wa mataifa inasema kuna hatari ndogo kwamba michuano ya olimpiki ya mwezi Agost inaweza kusambaza Zika kimataifa.

Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi na klabu ya Barcelona, Johan Cruyff amefariki dunia kwa ugonjwa wa kansa akiwa na miaka 68

Cruyff amefariki leo huko Barcelona nchini Hispania akiwa amezungukwa na familia baada ya kusumbuliwa na kansa ya mapafu.

Cruyff alijitokeza kuwa mmoja wa wachezaji mahiri duniani mwanzoni mwa miaka ya 1970 alipoisaidia klabu yakke ya Ajax Amsterdam kushinda mataji matatu ya Ulaya mfululizo kuanzia mwaka 1971 hadi 1973 na akatajwa uwa mchezaji bora wa mwaka wa bara la Ulaya kwa miaka ya 1971, 1973 na 1974.

Alijiunga na Barcelona kwa ada ya rekodi ya dunia kwa kipindi hicho ya dola milioni 2.0 na ndipo hapohapo nyota huyo alifanikiwa kuwaongoza Barca kutwaa taji la kwanza  la La Liga baada ya miaka 15, mwaka 1974. Lakini pia mwaka huohuo wa 1974, Cruyff aliisaidia timu yake ya taifa ya Uholanzi kufika fainali ya kombe la dunia.

Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu Johan Cruyff. Amen

Kampuni inayoongoza katika teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) duniani ya HUAWEI imetangaza uteuzi wa mwanasoka bora wa dunia na mshambuliaji wa klabu ya FC Barcelona Lionel Messi kuwa balozi wake ambapo shirikiano huo kati ya Messi na Huawei, unaonyesha jinsi gani kampuni hiyo nguli duniani ilivyojipanga kuunganisha mwanasoka bora duniani, nabidhaa bora duniani.

methi 3

Akizungumzia uteuzi huo, mkurugenzi mtendaji wa Huawei kanda ya Afrika Peter Hu alisema “Tuna furaha kutangaza ushirikiano na mwanasoka mwenye kipaji cha kipekee anayewatia moyo mamilioni ya watu duniani kufata ndoto zao, kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo na kuwa na mafanikio kila siku. Messi anaamini katika ubora wa bidhaa na huduma zaHuawei, kama sisi, naye daima anatafuta fursa za kufikia ubora zaidi.”

Akizungumzia ushirikiano huo, Lionel Messi alisema “Ni lazima upambane ili kufikia ndoto zako, ni lazima ujitoe haswaa, daima ukitazama mbele ili kufikia ubora unaoutaka. Siku unayodhani kuwa hakuna mabadiliko zaidi, ni mwanzo wa kuanza upya kufikia mafanikio mengine”

Akizungumzia uwekezaji wa Huawei barani Afrika, Hu alisema “Dhamira ya Huawei kwa bara la Afrika inaweza kuonekana kwa kutazama kiasi gani Huawei zinabadili maisha ya waafrika. Katika ukanda wa Africa kusini na mashariki mwaAfrika, Huawei inashikilia namba mbili (2) kwa usambazaji wa simu janja (Smartphones). Kwa upande mwingine, tafiti za masoko zinaonyesha kuwa, Huawei inashikilia karibu asilimia 15% ya simu janja zote katika ukanda huo. Pia tunaendelea kuleta na kusambaza zaidi simu za kiwango cha juu, kwa mfano Huawei P8 Lite ilishinda tuzo hivi karibuni nchini Afrika ya Kusini.”

methi2

“Lionel Messi atasaidia watu wengi zaidi, hasa waafrika kuzingatia, kuwa na subirá na uvumilivu na baadaye kufanikiwa kuunganishwa na UKUU.  Kwa kuunganisha ukuu, sisi kama Huawei, tunaonyesha shauku zetu kwa wateja wetu ” alihitimisha, Hu.