Habarika | MBUNGE AWATAKA WANAWAKE KUWANYIMA UNYUMBA WAUME ZAO MPAKA WAONYESHE VITAMBULISHO VYA KUPIGIA KURA
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

MBUNGE AWATAKA WANAWAKE KUWANYIMA UNYUMBA WAUME ZAO MPAKA WAONYESHE VITAMBULISHO VYA KUPIGIA KURA

Katika hali isiyo ya kawaida mbunge mmoja nchini Kenya amewakataza wanawake wa nchi hiyo kukutana kimwili na waume zao ili kuwabana kwenda kujiandikisha katika daftari la uchaguzi mkuu.

Mbunge huyo wa Mombasa, Misho Mboko amesema njia pekee ya kuwabana wanaume kwenda kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Kenya utakaofanyika mwezi Agosti ni kukataa kushiriki tendo la ndoa hadi wawaonyeshe vitambulisho vya kupigia kura.

“Wanawake hii ni mbinu ambayo mnatakiwa kuitumia, ni njia nzuri. Mkatae kufanya nao mapenzi hadi wawaonyeshe kadi zao za kupigia kura,” alisema Mboko.

Mboko ametumia mbinu hiyo ili wanaume wengi wajitokeze kupiga kura kwa kujiandikisha mapema na kupata vitambulisho kabla ya zoezi la kuandikisha wapiga kura kufungwa Februari, 17.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook8Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By