Habarika | MAUAJI YA WAUMINI WATATU WA JUMUIYA YA WAISLAM YA WAHAMADIYA YALAANIWA VIKALI HUKO MWANZA
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

MAUAJI YA WAUMINI WATATU WA JUMUIYA YA WAISLAM YA WAHAMADIYA YALAANIWA VIKALI HUKO MWANZA

Jumuia ya waislamu Wahamadiya mkoani Shinyanga wamelaani vikali tukio la mauaji ya kinyama lililotokea msikitini katika mkoa wa Mwanza ambapo watu watatu walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa tukio ambalo linadhaniwa limelenga kuvuruga amani baina ya waumini wa dini hiyo na dini zingine.

Akitoa kauli ya kulaani mauaji hayo mjini Shinyanga katika mkutano ulioandaliwa maalum kwa ajili ya kuiombea nchi amani mbashiri mkuu wa jumuia ya Wahamadiya Tanzania, Bw.Tahir Mahamod Chautry amesema kilichotokea Mwanza hakiwezi kuvumilika huku akikemea baadhi ya watu wanaotumia neno jihad tofauti maana halisi ya neno hilo na kudai kuwa hata vitabu vitakatifu vya dini Quraan na Biblia hakuna hata sentensi moja inayomruhusu binadamu kumuua binadamu mwingine.
Nao baadhi ya wananchi walioshiriki katika mkutano huo wamelaani mauaji ambayo yamekuwa yanatokea mara kwa mara katika maeneo ya mikoa ya kanda ya ziwa na wameitaka serikali kufanya ulinzi shirikishi na wananchi kwakuwa wahalifu hutokaea ndani ya makundi ya raia huku baadhi ya watendaji wa serikali katika ngazi ya vijiji na kata wakidai kuwa wajibu wa viongozi wa dini na serikali ni kushikilia amani na utulivu wa raia wanaowaongoza.
Kwa upande wake mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bw.Mohamed Nchira amevitaja baadhi ya vyanzo vinavyosababisha uvunjifu wa amani na mauaji ya kinyama nwanayofanyiwa watu wasio na hatia huku akidai kuwa serikali haitafumbia macho matukio kama hayo yanayofanywa na watu wasiotaka kuishi kwa amani.
-ITV
Sambaza Makala hii: Share on Facebook3Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By