Habarika | MAREKANI YAIPUUZA KOREA KASKAZINI JUU YA USITISHWAJI WA MAZOEZI YA KIJESHI
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

MAREKANI YAIPUUZA KOREA KASKAZINI JUU YA USITISHWAJI WA MAZOEZI YA KIJESHI

Rais wa Marekani Barack Obama amepuuzilia mbali pendekezo la Korea Kaskazini la kuitaka Marekani isitishe mazoezi ya pamoja ya kijeshi na Korea Kusini.

Korea Kaskazini imesema itasitisha mpango wake wa kufanyia majaribio silaha za kinyuklia iwapo Marekani itasitisha mazoezi hayo ya kila mwaka.

Akiongea na wanahabari, Bw Obama alisema Marekani haichukulii pendekezo hilo kwa uzito na Pyongyang “itahitajika kufanya zaidi kushinda hilo”.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Korea Kaskazini Ri Su-yong ndiye aliyetoa ofa hiyo kwa Marekani wakati wa mahojiano nadra sana na wanahabari

Mazoezi ya kila mwaka ambayo hufanywa na Marekani na Korea Kaskazini kila wakati huongeza uhasama baina ya nchi hizo mbili na Korea Kaskazini.

Bwana Ri alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya taifa lake kutangaza kwamba lilikuwa limefanikiwa kufyatua kombora la masafa marefu kutoka kwa nyambizi yake baharini.

Umoja wa Mataifa ulishutumu majaribio hayo ukisema ni ukiukaji mkubwa wa maazimio ya awali ya umoja huo ya kuzuia mipango ya Korea Kaskazini kuwa na silaha za nyuklia.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook1Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By