Habarika | MAKONDA AMUWAJIBISHA RAIS MAGUFULI
layout-wrap boxed
Sunday, February 25, 2018

MAKONDA AMUWAJIBISHA RAIS MAGUFULI

Rais John Magufuli amekuwa mtu wa kwanza kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuhakiki silaha baada ya bunduki zake mbili aina ya Shot gun na bastola kuhakikiwa nyumbani kwake Ikulu, Dar es Salaam

Uhakiki huo umefanywa na maofisa wa Jeshi la Polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa kazi hiyo, Rais Magufuli alimpongeza Makonda na Jeshi la Polisi kwa kuendesha uhakiki wa silaha na alitoa mwito kwa watu wote wanaomiliki silaha nchini kuhakiki silaha zao na muda huo utamalizika Julai Mosi mwaka huu.

Rais Magufuli pia alilitaka jeshi la Polisi kuongeza juhudi za kukabiliana na watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ili kutokomeza kabisa vitendo hivyo

” Ni aibu kumuona askari Polisi mwenye silaha ananyang’anywa silaha, ni aibu na nasema hiyo ni aibu, mpaka jambazi akunyang’anye silaha na wewe una silaha?” Amehoji Rais Magufuli

Naye Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, kamishna Sirro alimshukuru Rais Maufuli kwa kuunga mkono kazi hiyo na alisema Polisi imejipanga kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa mafanikio.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone


Warning: file_get_contents(http://graph.facebook.com/?ids=http://habarika.com/makonda-amuwajibisha-rais-magufuli/): failed to open stream: HTTP request failed! HTTP/1.1 403 Forbidden in /home/habarika/public_html/wp-content/themes/habarika/elements/element.php on line 80
0 comments

By