Habarika | MAHAKAMA YAMFUTIA SHTAKA ALIYEKUWA KAMISHNA WA TRA NA WENZAKE WAWILI
layout-wrap boxed
Sunday, February 25, 2018

MAHAKAMA YAMFUTIA SHTAKA ALIYEKUWA KAMISHNA WA TRA NA WENZAKE WAWILI

Mwanzoni mwa mwezi huu April 01 2016 aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Harry Kitilya, Mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996 na  Afisa mwandamizi wa benki ya Stanbic tawi la Tanzania Shose Sinare na Sioi Solomoni walipandishwa kizimbani kwa tuhuma zilizokuwa zikiwakabili zikiwemo za kula njama kutenda kosa pamoja na kosa la kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kesi hiyo kupigwa kalenda tarehe 22 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kupangwa kusikilizwa tena leo tarehe 27 April, imesikilizwa na mahakama imetoa maamuzi juu ya baadhi ya mashtaka.

Korti Kisutu, Dar es Salaam imefuta shtaka la kutakatisha fedha dhidi ya aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Harry Kitilya na wenzake 2. Mawakili wa watuhumiwa hao sasa wanaomba dhamana ili watuhumiwa hao wasirejeshwe tena rumande.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook1Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By