Habarika | MAGUFULI AWAASA WASHIRIKI WA KINYANG'ANYIRO CHA UMEYA DAR KUKUBALI MATOKEO
layout-wrap boxed
Sunday, February 25, 2018

MAGUFULI AWAASA WASHIRIKI WA KINYANG’ANYIRO CHA UMEYA DAR KUKUBALI MATOKEO

Rais John Magufuli amezitaka pande zinazogombea kiti cha Umeya katika jiji la Dar es Salaam, kukamilisha mchakato wa kumpata Meya katika uchaguzi uliopangwa kufanyika leo badala ya kuendelea kulumbana

Dr. Magufuli alisema upande wowote uwe tayari kupokea matokeo ya uchaguzi huo ili Meya apatikane na jiji liweze kuendelea na mipango yake ya kuwahudumia wananchi bila vikwazo

“Mahali tunapostahili kushinda kama tumeshinda tushinde kweli, lakini mahali tunaposhindwa napo tukubali kushindwa na hiyo ndio demokrasia ya kweli” aliongeza Rais Magufuli

WAKATI HUOHUO

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali ombi la kuzuia uchaguzi wa umeya na unaibu wa jiji la Dar es Salaam unaotarajiwa kufanyika leo na kuamuru uchaguzi huo ufanyike kama ulivyopangwa

Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Warialandwe Lema kwa kuwa Mahakama imeona hakuna sababu zozote za msingi zilizowasilishwa na mlalamikaji kuzuia uchaguzi huo

Aidha alisema kulikuwa na kasoro nyingi ikiwemo kukosekana kwa orodha inayoonyesha majina ya wapiga kura jambo lililosababisha Mahakama kutokujua kama waleta maombi ambao ni Suzan Massawe na Kumjhi Mohammed kupitia wakili wao  Elias Nwela kama ni miongoni mwa wapiga kura ambapo awali walalamikaji hao walidai kuwa hawajapewa haki yao ya kushiriki katika uchaguzi huo.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone


Warning: file_get_contents(http://graph.facebook.com/?ids=http://habarika.com/magufuli-awaasa-washiriki-wa-kinyanganyiro-cha-umeya-dar-kukubali-kushindwa/): failed to open stream: HTTP request failed! HTTP/1.1 403 Forbidden in /home/habarika/public_html/wp-content/themes/habarika/elements/element.php on line 80
0 comments

By