Habarika | MAGUFULI AAHIDI KUPUNGUZA KODI KATIKA MISHAHARA KWA WAFANYAKAZI
layout-wrap boxed
Sunday, February 25, 2018

MAGUFULI AAHIDI KUPUNGUZA KODI KATIKA MISHAHARA KWA WAFANYAKAZI

Rais wa Tanzania John Magufuli ameahidi kwamba kuanzia bajeti ijayo kodi katika mishahara kwa wafanyakazi itapungua kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 10 au 9.

Aidha, amesema ataweka kiwango cha kima cha juu na kwamba wale wote wanaopokea mishahara ya hadi shilingi milioni 40, itapunguwa na haitazidi milioni 15

Rais Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara Kaskazini Magharibi mwa Tanzania (Wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita) ambapo amewataka wananchi wafanye kazi kwa bidii ili kuondokana na tabia ya utegemezi wa misaada ya nje.

“Ni lazima tujisimamie sisi wenyewe. Na tukijisimamia sisi wenyewe kwa kila mmoja kuwajibika mahali alipo, kama ni mfanyakazi afanye kazi kwelikweli. Kama ni mkulima afanye ukulima kweli kweli, kama ni mfanyabiashara afanye biashara kweli kweli, kama ni mfugaji afuge kweli kweli, kama ki mvuvi avue kweli kweli, Tanzania hii tutavuka,” amesema Magufuli.

 

Sambaza Makala hii: Share on Facebook3Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By