Habarika | MAFURIKO YAACHA KAYA 10 BILA MAKAZI MKURANGA
layout-wrap boxed
Tuesday, December 12, 2017

MAFURIKO YAACHA KAYA 10 BILA MAKAZI MKURANGA

mafuriko

Kaya kumi zilizomo katika kijiji cha Kipaka, wilayani Mkuraga, Pwani, zimeachwa bila makazi baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko.

Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, alizitembelea familia hizo ili kuwajulia hali na kuwapa pole, alijionea hali hiyo na kuagiza nini kifanyike ili kuwanusuru iwapo mvua zitanyesha tena huku akiwapa vyakula, mafuta ya kupikia na sabuni.

Waathirika wa mafuriko hayo walisema maji yaliyosababisha mafuriko yalitoka barabara ya Kilwa iliyojengwa na wakala wa barabara Tanzania (TANROADS), ambapo matoleo ya maji ya barabara hiyo huelekezwa kwenye makazi ya watu.

Wananchi hao pia walimweleza mbunge  huyo tatizo la kiwanda cha Bakhresa kilichojengwa na kuzuia maji kupita katika mkondo wake.

DIwani wa mwandege, Adolf kowelo, alimshukuru mbunge huyo kwa kuwajali wananchi wake huku akisema ulinzi na usalama katika kitongoji cha kibelewele umepungua na kusababisha wizi kutokea mara kwa mara.

-TANZANIA DAIMA

Sambaza Makala hii: Share on Facebook5Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By