Habarika | LUKUVI AAGIZA WATUMISHI MONDULI KUFIKISHWA KORTINI
layout-wrap boxed
Sunday, February 25, 2018

LUKUVI AAGIZA WATUMISHI MONDULI KUFIKISHWA KORTINI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameagiza watumishi watatu wa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya wilaya ya Monduli kupandishwa kizimbani kutokana na tuhuma za wizi wa fedha za halmashauri hiyo ambapo watumishi hao wanadaiwa kuuza viwanja zaidi ya 200 kati ya Sh milioni mbili hadi nne bila kuingiza fedha hizo katika akaunti ya halmashauri hiyo.

Lukuvi alitoa agizo hilo juzi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Franciz Miti kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake wilayani humo baada ya wananchi kutoa malalamiko yao ya kuuziwa viwanja hewa na watumishi wa halmashauri.

Watumishi wanaotuhumiwa ni Ofisa Ardhi Mteule wa wilaya hiyo, Kitundu Mkumbo ambaye ni mpimaji wa ardhi, Leonard Haule pamoja na Mchora Ramani, Leonard Mkwavi.

Lukuvi alisema kuwasimamisha kazi watumishi hao haitoshi hivyo ni yema wakafikishwa mahakamani kwa kukiuka maadili ya watumishi wa umma pamoja na kurudisha fedha zote za wananchi hao waliowatapeli kwani wanalipa stakabadhi za halmshauri

Aisha aliagiza ofo ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (Takukuru) kwa kushirikiana na polisi katika wilaya hiyo kufanya uchunguzi wa haraka na wa kina kisha kuwafikisha mahakamani watumishi hao

Akipokea maagizo hayo, Mkuu huyo wa wilaya alisema baada ya kutambua ubadhilifu huo aliagiza watumishi hao kuwekwa ndani kwa saa 24 pamoja na kuwasimamisha kazi. Alisema uchunguzi huo umeshaanza na kwamba uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani mara moja

Sambaza Makala hii: Share on Facebook2Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like


Warning: file_get_contents(http://graph.facebook.com/?ids=http://habarika.com/lukuvi-aagiza-watumishi-monduli-kufikishwa-kortini/): failed to open stream: HTTP request failed! HTTP/1.1 403 Forbidden in /home/habarika/public_html/wp-content/themes/habarika/elements/element.php on line 80
0 comments

By