Habarika | KUHUSU
layout-wrap boxed
Sunday, February 25, 2018

KUHUSU

Habarika ni forum inayokuweka karibu zaidi na michezo yote uipendayo kitaifa na kimataifa kwani tunahakikisha unapata habari motomoto kwa wakati muafaka ili kukata kiu yako ya kuhabarika kimichezo. Hutahabarika tu, lakini pia utapata fursa ya kuongeza ufahamu wako kuhusu michezo.Ikiandaliwa na watu wenye ujuzi na ufahamu wa hali ya juu katika michezo bila ya kubagua aina ya mchezo, Habarika inakupa maudhui ya kimichezo ambayo huwezi kuyapata kwingine kokote kwa lugha ya Kiswahili ambayo wewe mwanamichezo ungetamani kupata kuyasikia au kuyaona. Hatuishii tu kukupa habari za kimichezo kwani tunajua unataka kujua mengi zaidi ya habari, na ndio maana utakapoichagua Habarika utapata kifurushi kamili kitakachokuwezesha kuimaliza siku yako ukiwa na ufahamu wa hali ya juu kwenye tasnia nzima ya michezo.Utapata makala na Uchambuzi,video mbalimbali za kimichezo zenye kukusisimua, utapata kuwajua wanamichezo mahiri katika michezo yote kwa hapa nyumbani na kimataifa ili uweze kujua wapi walipotoka, nini wamefanya na wapi wanatamani kufika na pia tapata kujua undani wa mashindano mbalimbali ya kimichezo yanayojiri duniani, bila kusahau matukio muhimu yaliyojiri ndani ya wiki nzima. Utakapoichagua Habarika utakuwa umechagua kuongeza ufahamu wako katika michezo, kitaifa pamoja na kimataifa, na huo ndio upekee tunaokuletea ambao umekuwa ukiuhitaji. Karibu tuongeze ufahamu kwasababu yapo mengi tusiyoyajua kuhusu michezo.Hii ndio Habarika, Ni michezo mwanzo mwisho.

 

By