Habarika | KUBENEA ANA KESI YA KUJIBU, YASEMA MAHAKAMA.
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

KUBENEA ANA KESI YA KUJIBU, YASEMA MAHAKAMA.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam imesema mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) anayekabiriwa na kesi ya kumtolea lugha ya matusi Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, ana kesi ya kujibu.

Uamuzi huo ulitolewa mahakamani hapo  na Hakimu Mkazi, Thomas Simba, anayesikiliza kesi hiyo baada ya upande wa mshtaka kufunga ushahidi wake.

Baada ya kusema hayo, Hakimu Simba alimhoji Kubenea kupitia wakili wake, Peter Kibatala, iwapo mshtakiwa huyo atatoa ushahidi kwa njia ya kiapo, bila kiapo ama kukaa kimya na wakili Kibatala alielea kuwa mshtakiwa atajibu kwa njia ya kiapo. Kesi imeahirishwa hadi Mechi 7, ambapo mshtakiwa ataanza kujitetea na anatarajiwa kuwa na mashahidi wanne.

Kwa mujibu wa  sheria, endapo Kubenea atapatikana na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini isiyozidi Sh. Milioni moja ama adhabu zote kwenda pamoja.

Wakati wa usikiliwaji wa kesi hiyo, upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi watatu, akiwamo Makonda ambaye aliieleza mahakama kuwa alishangaa kuporomoshewa matusi na Kubenea walipokutana katika mgomo wa wafanyakazi wa kiwanda cha utengenezaji wa nguo cha Tooku.

Makonda alidai alishangaa kwa sababu maneno aliyoyatamka mbunge huyo hayakustahili kutamkwa na kiongozi kama yeye, kwa kuwa ni ya udhalilishaji, yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Katika kesi hiyo, Kubenea anadaiwa kuwa Desemba 14, mwaka huu katika kiwanda cha Tooku Garments Co. Ltd maeneo ya Mabibo External, Wilaya ya Kinondoni, alitumia lugha ya matusi dhidi ya Makonda

-TANZANIA DAIMA

Sambaza Makala hii: Share on Facebook4Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By