Habarika | KOREA KASKAZINI YAENDELEA KULIPUA MAKOMBORA YAKE KUELEKEA KOREA KUSINI
layout-wrap boxed
Thursday, September 21, 2017

KOREA KASKAZINI YAENDELEA KULIPUA MAKOMBORA YAKE KUELEKEA KOREA KUSINI

mako

Korea Kusini inasema kuwa majirani zao Korea Kaskazini kwa mara nyingine tena, wamewafanyia majaribio ya makombora mawili ambapo hiyo inaonekana kuwa ni hatua ya wazi ya kukiuka makubaliano hali ambayo itaulazimu Umoja wa mataifa kuliwekea taifa hilo vikwazo vya kiuchumi. Taarifa zasema kombora la kwanza halikufanikiwa huku la pili likisafiri umbali wa kilomita mia nne.

Msemaji wa Waziri wa Umoja wa taifa wa Korea Kusini Joeng Joon-hee amesema majaribio hayo ni kukiuka vikwazo.

“Ulipuaji huo wa makombora kwa kutumia Teknolojia ya angani unakiuka maazimio ya Umoja wa mataifa huku nia yao ikiwa ni uchokozi dhidi yetu. Tunashauri ni vyema kwa Korea Kaskazini kuzidisha nguvu katika kuimarisha amani katika eneo la rasi ya Korea na kwa maisha ya watu wake ambayo Korea kaskazini imekuwa ikiyahatarisha kila wakati.” Amesema

Naye waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe amelaani hatua hiyo ya Korea ya Kaskazini.

“Leo kumelipuliwa makombora kwa kutumia teknolojia ya angani iliyotumika zamani huu ni ukiukwaji wa wazi wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa. hatutaruhusu na tutaandaa azimio la kupinga hatua hiyo,” amesema Waziri Mkuu huyo

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn1Share on Google+0Email this to someone

You may also like


Warning: file_get_contents(http://graph.facebook.com/?ids=http://habarika.com/korea-kasakazini-yaendelea-kulipua-makombora-yake-kuelekea-korea-kusini/): failed to open stream: HTTP request failed! HTTP/1.1 403 Forbidden in /home/habarika/public_html/wp-content/themes/habarika/elements/element.php on line 80
0 comments

By