Habarika | KESI YA MCHINA MUUZA PEMBE ZA NDOVU 'MALKIA WA PEMBE' YAAHIRISHWA
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

KESI YA MCHINA MUUZA PEMBE ZA NDOVU ‘MALKIA WA PEMBE’ YAAHIRISHWA

Kesi dhidi ya mwanamke mfanyabiashara raia wa China anayetuhumiwa na mashtaka ya kuendeleza mtandao wa kihalifu wa ulanguzi wa pembe barani Asia imeahirishwa kwa wiki mbili nchini Tanzania.

Waendesha mashtaka wanasema Yang Feng Glan, anayejulikana kwa umaarufu pia kama Malkia wa pembe, anaendesha biashara haramu ya kuwaua ndovu katika mbuga za wanyama ili kupata pembe zao ambazo wanazisafirisha na kuziuza katika mataifa ya bara Asia.

Yang ambaye alifikishwa mahakamani Jumatatu asubuhi mjini Dar es Salaam anashutumiwa kwa kuendeleza shughuli hiyo kwa takriban miaka 14 licha ya kukana mashtaka hayo

Maafisa wa serikali Tanzania wametaja kukamtwa kwa Yang Feng Glan mnamo Oktoba mwaka jana kama ufanisi mkubwa. Tanzania imepoteza thuluthi mbili za ndovu wake katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook1Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By