Habarika | KAULI YA ZUBEIR ALI MAULID BAADA YA KUCHAGULIWA KUWA SPIKA MPYA Z'BAR HII HAPA..
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

KAULI YA ZUBEIR ALI MAULID BAADA YA KUCHAGULIWA KUWA SPIKA MPYA Z’BAR HII HAPA..

“Nawashukuru sana wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kunipigia kura na kupata ushindi mkubwa ambapo naahidi kufanya kazi kwa ajili ya kuleta maendeleo ambapo mafanikio yote hayo ni mashirikiano kwenu ninyi”,

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi (BLW) wamemchagua kwa kura za kishindo Spika mpya Zubeir Ali Maulid kwa kura 75 kuwa Spika wa Nne wa Baraza hilo.

Maulid amewataka wajumbe wajumbe wa baraza kufanya kazi kwa uadilifu kuhakikisha wanasimamia serikali kuona inawajibika kwa ajili ya kuleta maendeleo licha ya kwamba Baraza hilo linaundwa na wajumbe wote kutoka chama tawala, CCM

Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Dk Yahya Khamis Hamad alitangaza matokeo hayo yaliyotokana na wajumbe wa BLW kupiga kura ambazo kura 75 zilimchagua Maulid huku kura moja ikisema Hapana.

Maulid alikula kiapo cha utii na uaminifu kwa ajili ya kazi za Spika wa BLW na kuahidi kuleta mabadiliko makubwa katika chombo hicho ambacho kipo kwa ajili ya maslahi ya wananchi wa Zanzibar na kuwatumikia. Na baada ya hapo alikabidhiwa katiba zote mbili za serikali ya Mapinduzi Zanzibar na ile ya Muungano pamoja na kanuni zinazosimamia utekelezaji wa kuendesha Baraza la Wawakilishi kutoka kwa Katibu wa Baraza.

Maulid anakuwa Spika wa Nne akitanguliwa na Idriss Abdul Wakil na Ali Khamis (wote marehemu) na baadaye Pandu Ameir Kificho ambaye hivi karibuni alishindwa na Maulid katika uteuzi wa ndani ya CCM baada ya kuishikilia nafasi hiyo kwa miaka 20.

 

 

Sambaza Makala hii: Share on Facebook1Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By