Habarika | KAMPENI ZA URAIS MAREKANI: KASHFA YA MAUAJI YA LIBYA YAMKUMBA CLINTON, HUKU TRUMP NAYE AKIZUA UTATA
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

KAMPENI ZA URAIS MAREKANI: KASHFA YA MAUAJI YA LIBYA YAMKUMBA CLINTON, HUKU TRUMP NAYE AKIZUA UTATA

Wazazi wa wamarekani wawili waliouliwa miaka minne iliyopita nchini Libya wanamshutumu mgombea Urais kupitia chama cha Democratic Hillary Clinton ambaye alikuwa Waziri wa mambo ya nje wa Marekani kwa kuchangia kutokea kwa mauaji kipindi ubalozi wa Marekani nchini Libya uliposhambuliwa

Patricia Smith na Charles Woods, ambao ni wazazi wa Sean Smith na Tyrone Wood wamesema kuwa matumizi ya barua pepe binafsi zilichangia mauaji ya watoto wao.

Msemaji wa kampeni za Hilary Clinton amepinga tuhuma hizo. Ingawa kamati ya Chama cha Republican inaweka wazi mabaya aliyoyatenda Hilary, jambo linalotia doa kampeni zake za Urais.

Uvamizi wa majeshi ya kiislam katika ubalozi wa Marekani uliwauwa raia wanne wa nchi hiyo akiwemo Balozi Chris Stevens.

 

Wakati huko kwingineko……..

Mgombea Urais wa chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, amezua mjadala mpya baada ya kuwahimiza wafuasi wake wenye bunduki kumzuia mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton, kubatilisha haki yao ya kikatiba ya kumiliki silaha.

Bw Trump alikuwa akihutubu katika mkutano wa siasa katika jimbo la North Carolina ambapo amesema kuwa endapo Bi Clinton atashinda basi atateua majaji wa Mahakama ya Juu ambao watafanikisha kuondolewa kwa haki ya raia kumiliki bunduki huku Trump akisisitiza kwamba ni hatua ya raia pekee, ambayo inaweza kuzuia hilo lisifanyike.

Maafisa wa kampeni wa Clinton wameshutumu matamshi ya Trump na kusema kuwa ni ya hatari huku washauri wa Trump wakisema kuwa alikuwa tu anawahimiza watu wanaoamini katika haki ya raia kumiliki silaha watumie kura zao kufanya uamuzi.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By